Dimitar Berbatov |
Mshambuliaji
wa Manchester United Dimitar Berbatov ametoa
kauli akisema ni bora kuondoka katika klabu hiyo.
Berbatov
ambaye ameitumikia klabu hiyo michezo 21 tu amekuwa si chaguo tena la meneja wa
klabu hiyo Sir Alex Ferguson.
Sasa raia
huyo wa Bulgaria ambaye alinunuliwa kwa gharama ya pauni milioni £30.75 mwaka 2008
anasema ni bora aondoke akatafute timu ambayo atakuwa na uhakika wa kucheza
katika kikosi cha kwanza.
"naipenda
hii klabu , lakini ni wazi kuwa haifai kwa mtu yoyote kama hupati nafasi ya
kucheza," Berbatov amekaririwa kupitia mtandao wake.
“nataka kucheza ,nataka kutoa huduma lakini
bila ya sababu ya kueleweka hilo halitokei hivyo kwa yoyote ni inakuwa bora
kusema goodbye.”
Berbatov aliifungia
United jumla ya mabao 14 katika msimu wake wa kwanza akitokea Tottenham alikuwa
pia katika mchezo wa fainali wa Champions League ambapo walichapwa
na Barcelona.
No comments:
Post a Comment