KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, July 26, 2012

Hatimaye Chelsea yakamilisha usajili wa Oscar


Chelsea imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Oscar  na kuingia nae mkataba wa miaka mitano kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni £25m.
Mbrazil huyo ambaye kwasasa yuko nchini Uingereza kwenye michuano ya Olympic akiwa na kikosi cha Brazil anajiunga na Chelsea akitokea Internacional na huko nyuma alikuwa akiitumikia Sao Paulo.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20 amekuwa akifananishwa na mbrazil mwenzake Ricaldo Kakal.
Mabingwa hao wa vilabu ulaya Chelsea tayari wameshakamilisha usajili wa Marko Marin na ndugu wawili Eden na Thorgan Hazard majira haya ya uhamisho wa kiangazi.

Oscar huko nyuma aliarifiwa kusubiri mpaka kumalizika kwa Olympics kabla ya kuakmisha taratibu za usajili kujiunga na kikosi cha Roberto Di Matteo lakini inaonekana mambo yameharakishwa tofauti na ilivyokuwa imepangwa.

No comments:

Post a Comment