KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, July 26, 2012

Liverpool 1-2 Roma: Adam afunga bao la kutoa machozi mchezo wa kwanza wa pre-season wa Liverpool.


Liverpool imeanza vibaya mchezo wa kwanza wa kujiandaa na msimu mpya wa ligi baada ya kuchapwa kwa bao 2-1 na Roma ya Italia mbele ya mashabiki waliojazana katika uwanja wa Fenway Park.
mashambulizi mawili ya kipindi cha pili kupitia kwa Michael Bradley na Alessandro Florenzi yalidhihirisha kuwa Giallorossi wako sawa licha ya jitihada za dakika za mwisho za Liverpool kupitia kwa kiungo Charlie Adam.
Bosi wa Liverpool Brendan Rodgers aliamua kuwatumia katika kikosi cha kuanzia Raheem Sterling na Nathan Eccleston sehem ya ushambulizi wakati wazoefu Martin Skrtel, Jamie Carragher na Joe Cole wakiwa sehemu ya kiungo. Wakongwe Francesco Totti na mshambiliaji Pablo Osvaldo walianza kwa upande wa Roma huku Zdenek Zeman akionekana kuwa imara katika kikosi hicho.
 

No comments:

Post a Comment