KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, August 29, 2012

KIMATAIFA:Coentrao nje michezo minne, kukosa pia Supercopa Clasico na Maicon huenda akabaki Inter


Coentrao nje michezo minne, kukosa pia Supercopa Clasico

Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho atalazimika hii leo kukosa huduma ya mlinzi wake wa kushoto Fabio Coentrao kufuatia shirikisho la soka nchini Hispania kumfungia mlinzi huyo kwa michezo minne kutokana na kupewa kadi nyekundu katika mchezo ambao Madrid walifungwa na Getafe mabao 2-1 mchezo uliopigwa jumapili iliyopita.
Coentrao alimwita mwamuzi Miguel Angel Perez Lasa mtoto wa malaya  katika mchezo huo na kamati ya nidhamu imeamua kumfungia kucheza kwa michezo minne .
Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 24 atakosa michezo ya ligi ya Hispania La Liga dhidi ya Granada, Sevilla, Rayo Vallecano pia mchezo wa marudiano wa Spanish Supercopa hii leo.
Aidha kocha wa Barcelona Tito Vilanova amesimamishwa kuketi katika benchi la ufundi kwa michezo miwili kufuatia kwenda kinyume na nidhamu ya benchi inavyotaka katika mchezo dhidi ya Osasuna uliopigwa jumapili.
Vilanova mwenye umri wa miaka 42 alionekana mara kadhaa katika mchezo huo akilalama kwa hasira juu ya maamuzi ya mwamuzi wakati mchezo ukiendelea licha ya kuonywa na mwamuzi msaidizi, ambapo aliondoshwa katika benchi na mwamuzi wa mchezo kunako dakika ya 70 ya mchezo huo.
Hata hivyo msaidizi huyo wa zamani wa Pep Guardiola atakosekana katika michezo dhidi ya Valencia na Getafe kwa kuwa kosa lake si kubwa kama ilivyo kwa Coentrao.

 Moratti: Maicon huenda akabaki Inter
Rais wa Inter Milan, Massimo Moratti ameweka wazi kuwa haoni sababu ya kwanini Maicon aihame klabu yake msimu huu wa uhamisho wa kiangazi.
Mlinzi huyo wa kulia wa kimataifa wa Brazil, bado ameendelea kuhusishwa na kutaka kuondoka Nerazzurri, na wakala wake akinukuliwa wiki iliyopita akisema kuwa vilabu kama Chelsea, Manchester City na Real Madrid vimekuwa vikionyesha nia ya kumsaini mlinzi huyo wa kulia.
Aidha wakati msimu wa uhamisho ukikaribia kufungwa huku Maicon akiachwa katika orodha ya wachezaji wa Inter kwenye kikosi kitakacho cheza dhidi ya Pescara ukiwa ni mchezo wa ufunguzi wa msimu wa Serie A, inaonekana wazi kuwa atasalia.
Alipoulizwa Morati na La Gazzetta Dello Sport juu ya Maicon na hatma yake ya baadaye alijibu "Maicon? Hebu tusubiri tuone nini kitatokea . Anaweza kusalia hapa na kufanya vizuri”.
 Kiongozi huyo wa juu wa Inter akaendelea mbele zaidi kwa kumsifia mchezajin wake mpya Antonio Cassano baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Pescara ambao Cassano ulikuwa ni mchezo wake wa kwanza ndani ya klabu hiyo.
"Nilimpenda alifanya vizuri katika mchezo dhidi ya Pescara. Ameonyesha kuwa yuko katika hari ya juu kimchezo na anatumia akili. Tumtumainiye kuwa ataendeleza hilo"
Inter kesho itakuwa ikicheza mchezo muhimu wa marudiano ukiwa ni mchezo wa Europa League ‘playoff’ dhidi ya dhidi ya Vaslui.

No comments:

Post a Comment