KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, August 30, 2012

KIMATAIFA:Terry na Gerrard warudishwa timu ya taifa ya England,Xavi: Barca ingeweza kuichapa Madrid licha ya kuwa pungufu,Martinez ana kazi kikosi cha kwanza Munich,Defoe aingia mkataba mpya na Spurs na Cesar anafikiria taji akiwa na QPR.


Terry na Gerrard warudishwa timu ya taifa ya England
 Meneja wa timu ya taifa ya England Roy Hodgson amewarejesha katika kikosi cha timu ya taifa ya John Terry na Steven Gerrard kwa ajili ya michezo miwili ya kuwania kufuzu fainali ya kombe la dunia dhidi ya Moldova na Ukraine.
Terry kwasasa anakabiliwa na uchunguzi toka chama cha soka cha England FA kufuatia tuhuma za kibaguzi msimu uliopita dhidi ya mlinzi wa QPR Anton Ferdinand na aliachwa katika kikosi kilichocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Itali.
Nahodha huyo wa Chelsea pamoja na kiungo mzoefu wa Liverpool Gerrard, wamerejeshwa kikosini lakini mshambuliaji wa Manchester United Wayne Rooney na mlinzi  Rio Ferdinand wameachwa kufuatia kusumbuliwa na majeraha.
Walinda mlango Jack Butland na John Ruddy, ambao waliitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi kilichocheza dhidi ya Italia wamejumuishwa tena wakiwa pamoja na mlinda mlango namba moja Joe Hart.
Katika upande wa ulinzi nyota vijana Ryan Bertrand na Kyle Walker wanaungana na Terry, Ashley Cole na Joleon Lescott, wakati ambapo katika sehemu ya kiungo Tom Cleverley ameendelea kusalia katika kikosi hicho baada ya kuonyesha kiwango katika mchezo dhidi ya Italia pamoja na Michael Carrick.
Ushambuliaji , Andy Carroll amechaguliwa tena na ataungana na Jermain Defoe, Danny Welbeck na Daniel Sturridge.

Xavi: Barca ingeweza kuichapa Madrid licha ya kuwa pungufu.
 
 Xavi anasema  Barcelona ilikuwa na nafasi ya kuichapa Real Madrid hapo jana licha ya kusalia 10 uwanjani na hilo lingewezekana hata kabla ya mapumzikoni ambapo  Adriano alitolewa kwa kadi nyekundu.
Catalans katika mchezo huo walifungwa mabao 2-1 mchezo uliopigwa Santiago Bernabeu, na kuwafanya Madrid kushinda Spanish Supercopa kwa faida ya magoli mawili ya ugenini ambapo Barca walifungwa mabao 3-2 kule Nou Camp.
Kama hiyo haitoshi kiungo huyo mwenye mvuto anapokuwa uwanjani alionyesha soka la kuvutia katika timu hasa katika kipindi cha pili.
Amenukuliwa akisema
"makosa mawili na kadi nyekundu yalitugharimu, ukiachana na hilo tulirudi kwenye mchezo vizuri na pengine tungeshinda Supercopa pamoja na kwamba tulikuwa 10"
"tuliendelea kucheza mpira wetu kwa style ya uchezaji wetu licha ya upungufu wetu. Kipindi cha pili tulitengeneza nafasi nyingi ambazo zingetuwezesha kushinda taji."
Hata hivyo amewataka wachezaji wenzake kusahau  Supercup na kurejea La Liga ambapo Barcelona watakuwa wenyeji wa Valencia jumapili.
 Martinez ana kazi kikosi cha kwanza Munich

Licha ya kutengeneza rekodi ya usajili katika soka la nchini Ujerumani , Javi Martinez anakabiliwa na vita kubwa ya kupata namba katika timu yake ya Bayern.
Mkurugenzi wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amenukuliwa akisema .
"kama atakuwepo katika kikosi dhidi ya Stuttgart jumapili hilo ni jukumu la kocha "
Tayari kuna ushindani mkubwa katika eneo la kiungo katika viunga vya Allianz Arena, huku pia changamoto kubwa ikiongezwa na Basque.
Moja ya sababu ya Martinez kukubali kujiunga na Bayern inaelezwa kuwa ni kuhakikishiwa kutumika kama mchezaji wa kiungo kuliko ulinzi ambayo alikuwa akichezea alipokuwa na Athletic Bilbao msimu uliopiota jambo ambalo lilikuwa likimkwaza.
Martinez, alii gharimu Bayern kitita cha euro milioni €40 ambacho atalazimika kupigana kweli kweli ili kupata nafasi ya kucheza katika nafasi hiyo ambayo ya kiungo mzuiaji ambapo kuna Bastian Schweinsteiger, Toni Kroos, Luiz Gustavo na Anatoli Tymoschtschuk ambao nao wanagombea nafasi hiyo.
Lakini Schweinsteiger ambaye hakuwa ni mwenye bahati kuelekea kumalizika kwa msimu sasa amerejea vizuri  na Martinez atalazimika kujenga 'great partnership' hiyo ikiwa ni kauli ya nguli katika soka la Ujerumani Franz Beckenbauer.
Hiyo inaweza ikawafanya Gustavo, ambaye alisajiliwa kwa euro milioni €17 akitokea Hoffenheim 19 mwezi uliopita pamoja Tymotschtschuk kuwa na makazi ya kudumu katika benchi.
  Defoe aingia mkataba mpya na Spurs

Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur Jermain Defoe ameingia mkataba mwingine na klabu yake hiyo ambao utamaliza minongono ya kuwa alikuwa katika mipango ya kuondoka White Hart Lane.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England alikuwa akifikia ukiongoni kwa muda chini ya kocha wa zamani wa Spurs Harry Redknapp lakini akaahidiwa kipindi kingine na maisha ndani ya klabu hiyo na Andre Villa-Boas.
Defoe amenukuliwa kupitia katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter akisema
"ni wiki nzuri kwa nimesaini mkataba mpya na spurs & na kujumuishwa katika kikosi cha England kwa ajili ya michezo muhimu #goalsgoalsgoals."
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amejumuishwa katika kikosi cha timu ya taifa ya England na kocha  Roy Hodgson kwa ajili ya michezo miwili ya kuwania kufuzu fainali ya kombe la dunia dhidi ya Moldova na Ukraine.
Defoe mwenyewe alisikika akisema kuwa katika mashaka juu ya hatma yake ya baadaye na Spurs kiasi kutangaza kuwa huenda akatafuta njia ya kuelekea endapo hata hakikishiwa nafasi katika kikosi cha kwanza.
Villas-Boas alikuwa akihusishwea na kutaka kuwasajili washambuliaji kadhaa wakiwemo Leandro Damiao, Loic Remy na Willian, lakini inaonekana hilo limezimwa na usajili wa Defoe, Emmanuel Adebayor na kinda Harry Kane.
 Cesar anafikiria taji akiwa na QPR
 Julio cesar aliyesajiliwa hivi karibuni na Queen's Park Rangers anaamini endapo wachezaji wenzake watajiamini basi wanaweza kutwaa taji la ligi kuu ya nchini ENGLAND.
Cesar,ambaye ana umri wa miaka 32, anaamini hakuna kisicho wezekana pale Loftus Road hasa ikizingatiwa kuwa ni kiasi kikubwa cha pesa kimeahidiwa kutolewa na mmiliki wa klabu hiyo Tony Fernandes kwa ajili ya kununua wachezaji wapya.
Amenukuliwa na Daily Mail akisema
"nina ndoto nyingi sana na QPR, kikubwa ni kucheza vizuri kwa ajili ya mashabiki, meneja , mwenyekiti na wewe mwenyewe".
Anasema endapo watafanya hivyo hatimaye watamaliza ligi katika nafasi nne za juu na kufuzu kwa ajili ya vilabu bingwa ulaya na baadaye siku zijazo kuna uwezekana wa kutwaa Premier League.
Cesar ametolea mfano kuwa ziku chache zilizo pita hakuna aliyedhani kuwa Manchester City ingeweza kutwaa taji la Premier League, Lakini ukiweka nia hilo linaweza kutokea.
Mlinda mlango huyo ametoa kauli hiyo baada ya kuona Rangers ikianza vibaya msimu lakini anadhani mambo yataimarika katika kikosi hicho cha kocha Mark Hughes.
Akiwa katika kikosi Rangers msimu huu, mlinda mlango huyo wa zamani wa Inter Milan anakabiliwa na ushindani mkubwa wa kukalia lango la timu hiyo kutoka kwa Rob Green.

No comments:

Post a Comment