KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, August 30, 2012

UJIO WA MBUYU TWITE KATIKA PICHA.

 
 
Mlinzi wa kimataifa wa klabu ya Yanga Mbuyu Twite amepata mapokezi makubwa hii leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati beki huyo alipowasili akitokea Rwanda.
Nyimbo za Mbuyu Mbuyu Mbuyu na kelele nyingine zikimbeza mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage zilisikika zikiimbwa  na mamia ya mashabiki wa Yanga wake kwa waume waliofurika uwanjani hapo kwaajili ya kumpokea beki huyo.
Mara baada ya kuwasili uwanjani hapo majira ya saaa10.30 jioni,Twite aliyepokewa na viongozi wa Yanga wakiongozwa na katibu mkuu,Selestine Mwesigwa alikabidhiwa jezi namba 4 yenye jina la Rage  kama ishara ya ushindi dhidi ya wapinzani wao Simba.
Mara baada ya kukabidhiwa jezo hiyo,Twite alizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa umati alioushuhudia uwanjani hapo ulimpa moyo wakuona jinsi mashabiki wanamjali.
Baada ya mahojiano na Wanahabari, Twite alipanda  gari dogo na moja kwa moja msafara ulioongozwa na mabasi madogo aina ya Coastal ulielekea makao makuu ya Yanga yaliyoko Mtaa wa Jangwani.
Twite anatarajiwa kuonekana dimbani kwa mara ya kwanza akiwa na jezi ya Yanga jumamosi uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam pale ambapo mabingwa hao wa kombe la Kagame watakapokuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Coast Union ya Tanga ukiwa ni mmoja ya michezo ya maandaliazi ya ligi kuu ya soka Tanzania. Bara.