KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, September 30, 2012

HAWA NDIO WAKALI WA AFRIKA KATIKA SOKA, MBWANA SAMATA NAYE YUMO. WAMISRI WANAMUITA MUUAJI WA WAMISRI 'EGYPTIAN SLAYER'


 Mshambuliaji mwenye umri wa miaka 20 raia wa Tanzania. Mshambuliaji huyu raia wa Tanzania amebatizwa jina na vyombo vya habari vya nchini Misri la ‘Egyptian Slayer’ (YAANI MUUAJI WA WAMISRI),  baada ya kufanikiwa kufunga goli katika kila mchezo dhidi ya vilabu vikubwa vya nchini humo Al Ahly na Zamalek.
Mshambuliaji huyo mpaka sasa amefanikiwa kutikisa nyavu mara sita katika michuano hii ya vilabu bingwa barani Afrika ambapo mabao 4 ni dhidi ya vilabu vya Misri.
Mabao 3 kati ya hayo akifunga kwa kichwa akionyesha ni namna gani alivyo hatari katika kuruka hewani.

 Abdel-Wahed El-Sayed - Zamalek (EGYPT)
Abdel-Wahed El-Sayed - Zamalek (EGYPT) mwenye umri wa miaka 35 ambaye pia ni raia wa Misri ameonyesha kiwango cha kuvutia licha ya kwamba timu iliambulia point moja kati ya points 15. Alikuwa ndiye pekee ambaye aliyevutia cha timu yake.
 ‘Simba wa Afrika’, kama alivyo batizwa jina na mashabiki wa Misri hususani wale wa timu yake ya alikuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha anatikisa nyavu za wapinzani hususani katika michezo ya ugenini.
Uwezo mkubwa alionyesha katika mchezo dhidi ya TP Mazembe uliochezwa Lubumbashi alidhihirisha wazi kuwa alikuwa ni hatari licha ya timu yake kupoteza kwa kufungwa mabao 2.
Sehemu ya ulinzi ya Zamalek tatizo na kuruhusu mashambulizi lakini Abdel Wahed alikuwa akipigana kusaka mabao.

 Olorundare Dele - Sunshine Stars (NIGERIA)
 Mshambuliaji huyu ana umri wa miaka 21 ambaye pia ni raia wa Nigeria.
Olorundare Dele mara zote amekuwa ni mshambuliaji hatari kwa wapinzani wa timu yake ya Sunshine Stars katika hatua hii ya vilabu barani Afrika.
Mshambuliaji huyu wakati mwingine amekuwa akitumika kama mshambuliaji wa pembeni na hiyo ndiyo sababu ambayo imepelekea kikosi cha wanigeria kuwa kizuri katika mashindano.
Sunshine Stars ambayo haina historia ya kuchukua taji lolote barani Afrika, ilifanikiwa kufika katika hatua ya nusu fainali katika michuano hii ya kwanza ya vilabu bingwa.
Akiwa ndiye mchezaji wa mchezo yaani “man of the match” katika mchezo dhidi ya ASO Chlef, Dele alifunga bao la kwanza na kutoa pasi ya mwisho iliyozaa goli na hivyo kuwapa ushindi vijana hao maarufu kama Agugu Boys na kupata points tatu muhimu.

 Franck Kom - Etoile du Sahel (TUNISIA)
Huyu ni kiungo raia wa Cameroon mwenye umri wa miaka 20 ambaye alikuwa akifanya kazi kubwa katika hatua ya makundi katika kikosi cha Etoile du Sahel.
Timu hii ya Tunisia ilishindwa kufuzu baada ya michezo yake minne ya hatua ya makundi kutokana na vurugu za mashabiki wake kuvamia uwanja katika mchezo dhidi ya wapinzani wao wakubwa Esperance.
Kom alitegemewa kuwa ni kiungo ambaye angeonyesha upinzani mkubwa katika sehemu ya kiungo baada ya kuonyesha soka la kueleweka. 

Soloman Asante - Berekum Chelsea (GHANA)
 Huyu ni mshambuliaji mwenye umri wa miaka 21 raia wa Ghana.
Hivi karibuni chama cha soka nchini Ghana kiliondoa mashaka juu ya uraia wa Solomon Asante baada ya kutoa taarifa kuwa ni halali kuichezea timu ya Taifa ya Ghana ‘Black Stars’.
 Asante alitumika katika kikosi cha timu ya taifa ya Bukina Faso miaka miwili iliyopita ukiwa ni mchezo wa kirafiki wakati huo akiichezea ASFA Yennenga, ambapo pia aliibuka kuwa mfungaji bora wa ligi kuu ya Bukina Faso ‘Burkinabé Premier League’ akiwa ana umri wa miaka 18.
Winga huyo wa kulia alikuwa na uwezo mkubwa wa kuingian ndani na kutoa msaada kwa Emmanuel Clottey, na kutengeneza nafasi za ushindi. Asnate alitajwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Ghana kwa ajili ya michezo dhidi ya Malawi na Liberia.

Mohammed Abou-Treika - Al Ahly (EGYPT)
 Akiwa na umri wa miaka 33 raia wa Misri licha ya kwamba imesali mwezi mmoja kabla ya kutimiza miaka 34, Abou-Treika anaonekana kupoteza uwezo wake wan soka wa ujana.
Kiungo huyu wa chini ameonyesha bado ana uzoefu mkubwa katika michuano hii, amefunga jumla ya magoli  6, Abou-Treika ndiye mfungaji mwenye magoli mengi katika kikosi cha Al Ahly katika michuano hii.
Alifanikiwa kufunga goli katika mchezo dhidi ya wapinzani wao wakubwa Zamalek na kuwaweka katika nafasi nzuri katika msiammo wa kundi
Abou-Treika aliendelea bado kuonekana gumzo licha ya kukosekana katika mchezo dhidi ya Berekum Chelsea, baada ya kuwa na majukumu mengine katika michezo ya  Olympic iliyofanyika nchini Engand.
Kwa bahati mbaya kwasasa , Treika amesimamishwa kwa miezi miwili na klabu yake ya Al Ahly kutokana na kugemea kucheza mchezo wa ‘Egypt Super Cup’ na huenda akakosekana katika michezo ya kumalizia michuano ya ligi ya mabingwa Afrika.

Yannick N’Djeng - Esperance Sportive de Tunis (TUNISIA)

 Mshambuliaji huyu ana umri wa miaka 22 ambaye ni raia wa Cameroon licha ya kwamba ana magoli 4 tu katika michuano hii lakini bado ameonekana kuwa ni hatari katika michuano hii ya vilabu na ngumu kuzuilika na mabeki.
N’Djeng mara nyingi huwa anafunga magoli ya dakika za mwisho, alifunga goli la pili la Esperance dhidi ya Sunshine Stars mchezo uliofanyika nchini Nigeria, lakini pia goli la dakika ya 93 dhidi ya ASO Chlef wakati ubao ukisomeka 2-2, na mwishowe na muhimu kuliko alifunga goli la pili dhidi ya Etoile du Sahel, bao ambalo lilisababisha mashabiki kuvamia uwanja muda mfupi baada ya N’Djeng kushangilia.

Walid Soliman - Al Ahly (EGYPT)
 Huyu ni winga mwenye umri wa miaka 27 raia wa Misri. Ni mjanja uwanjani na hii ni mara yake ya kwanza kucheza michezo hii ya vilabu bingwa.
Alifunga magoli mawili muhimu dhidi ya Berekum mchezo uliochezwa Cairo, katika mchezo dhidi ya Mazembe alitoa pande la pasi muhimu kwa Emad Metab aliyekunga goli la uongozi la Ahly, lakini pia kasi yake uwanjani katika mchezo dhidi ya Zamalek alikuwa mwiba kwa mlinzi wa kulia Ahmed Samir.
Soliman alikuwa ni mchezaji nyota wa mchezo dhidi ya Berekum Chelsea, wakati ambapo bosi wa zamani wa Chelsea Hans van der Pluijm akitanabaisha kuwa Soliman ndiye mchezaji wa mashindani na hutakiwi kukosa kumuangalia.

Tresor Mabi Mputu - TP Mazembe (DR CONGO)
 Huyu ni mshambuliaji raia wa Congo mwenye umri wa miaka 26 mara nyingine anafanishwa kama Samuel Eto’o mpya hasa baada ya kocha Claude le Roy kusema anaimani Mputu hana mlinzi wa kumzuia.
Mputu alikuwa nahodha wa Mazembe katika michuano ya vilabu bingwa Afrika 2009 na 2010 pamoja na kuonyesha kiwango safi katika fainali ya vilabu bingwa duniani.
Licha ya kufanya majaribio mara mbili katika klabu kubwa ya nchini England Arsenal bado , Mputu ameendelea kusalia Lubumbashi, ambapo ameendelea kuwa nyota baada ya adhabu ya kusimama miezi 12 kwa kuonyesha vitendo vya hovyo
Mputu amefunga mabao 6 mpaka sasa ikiwa ni pamoja kufunga mara mbili katika mchezo dhidi ya Berekum Chelsea, matokeo ambayo yameipeleka Mazembe katika nusu fainali.

Emmanuel Clottey - Berekum Chelsea (GHANA)

 Huyu ni mshambuliaji mwenye umri wa miaka  25 ambapo bila mashaka yoyote, Clottey anastahili kuongoza orodha hii ya wakali.
Akiwa na umri wa miaka 20 alikuwa ndiye mfungaji bora wa ligi ya Ghana ‘Glo Premier League’ akifunga jumla ya mabao 14.
 Baada ya kuhangaika huku na huko barani Ulaya ikiwa ni pamoja na kuelekea Austria na Denmark, kabla ya kurejea nchini Ghana, Clottey amerejea Afrika Magharibi.
Clottey kwasasa anaongoza kwa ufungaji katika ligi ya vilabu bingwa Afrika. Alifunga mabao matatu pekee yake yaani ‘hat trick’ dhidi ya Zamalek, na goli moja dhidi ya Ahly mjini Cairo, akaonyesha pia soka safi katika mchezo dhidi ya Mazembe mjini Lubumbashi.

No comments:

Post a Comment