Timu
ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys)
inaendelea vizuri na kambi ya mazoezi katika mikoa ya Mbeya na Njombe
ambapo leo jioni (Septemba 16 mwaka huu) itacheza mechi ya kirafiki
mjini Makambako na timu ya Manispaa.
Serengeti
Boys ambayo iko chini ya Kocha Jakob Michelsen na msaidizi wake Jamhuri
Kihwelo imeshacheza mechi nne mkoani Mbeya. Imecheza mechi hizo dhidi
ya Tanzania Prisons, Mbozi United, Mbeya City na Kombaini ya Kyela na
kupoteza moja tu.
Baada
ya mechi ya kesho (Septemba 17 mwaka huu) itacheza mechi ya mwisho
mkoani Njombe dhidi ya Kombaini ya Makambako na kurejea Dar es Salaam
siku inayofuata kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya mechi dhidi
ya Misri.
Mechi
hiyo ya kwanza ya raundi ya pili kuwania tiketi ya kucheza fainali za
Afrika kwa vijana zitakazofanyika Machi mwakani nchini Morocco itachezwa
Oktoba 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment