Waziri mkuu
wa zamani wa Italia ambaye pia ni Rais wa klabu ya AC Milan ya nchini humo Silvio Berlusconi amehukumiwa kwenda jela miaka minne
kutoka na ukwepaji wa kodi.
Berlusconi na
wenzie 10 walikuwa wakituhumiwa kununua haki za kampuni ya kimarekani ya filamu kwa
bei ya kutupa kupitia kampuni za nje wakati wa utawala wake kama waziri mkuu.
Waziri huyo
mkuu wa zamani wa Italia anatarajiwa kukata rufaa juu ya hukumu hiyo.
Katika usomwaji
wa hukumu hiyo aliunganishiwa kesi mbalimbali zinazohusu mambo ya kibiashara lakini
zilitupiliwa mbali kwa kigezo cha kwamba zilikuwa nje ya muda.
Wakati akisomewa
hukumu hii , waendesha mashitaka walidai kuwa sehemu ya pesa za kununulia haki
za filamu zilitumika katika uharamia wa kukwepa kodi kupitia kampuni yake ya Mediaset.
Mahakama imemuhuku
Berlusconi muda mrefu jela kuliko miaka mitatu na miezi nane kama ilivyoombwa
na waendesha mashtaka.
Habari zaidi zinakuja
No comments:
Post a Comment