KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, December 6, 2012

NDOTO YA LIONEL MESSI KUVUNJA REKODI YA GERD MULLER YA MABAO 85 KIPINDI CHA MWAKA MMOJA YATOWEKA.


Mshambuliaji nyota wa Barcelona Lionel Messi amejikuta akitolewa nje kwa machela kutokana na kupata maumivu makali katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Benfica.

Tito Vilanova hakumuanzisha mshambuliaji huyo kama ilivyo kawaida yake na kumuingiza katikati ya mchezo kipindi cha pili kwa lengo la kusukuma mashambuliaji zaidi.

Zikiwa zimesalia dakika tano mchezo huo kumalizika wakati huo matokeo yakiwa ni sare ya bila mabao, mshambuliaji huyo anayetazamiwa na wengi kushinda tuzo ya Ballon d'Or favorite aliwekwa chini na kuanza kulalamikia maumivu ya mguu wake kabla ya kutolewa nje ya dimba la Camp Nou kwa matibabu.

Maafisa wa Barcelona muda mfupi baadaye wakatumia mtandao wa kijamii wa twitter kwa kutoa ujumbe
"Messi amepatwa na mchubuko katika mguu wake wa kushoto . Anatakiwa kufanyiwa vipimo zaidi ukubwa wa jeraha lake,".

Baada ya mshambuliaji huyo kutolewa nje hakukuwa na mabadiliko yoyote ya matokeo na hivyo mchezo huo kumalizika kwa matokeo ya 0-0, matokeo ambayo yanaiondoa Benfica mashindano na kusogezwa katika Europa League wakati ambapo Celtic ikisonga mbele baada ya kuichapa Spartak Moscow.

Wengi walitazama kuwa usiku wa jumatano hii utakuwa ni usiku wa kihistoria kwa Messi kuvunja rekodi ya Gerd Muller ya kufunga magoli 85 katika kipindi cha mwaka mmoja.

Aidha majeraha ya Messi huenda yakamuweka nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki kadhaa mpaka katika kipindi cha majira ya baridi, hiyo ikimaanisha kuwa Messi atakuwa ameshindwa kuvunja rekodi hiyo ya mwasisi wa kijerumani Muller.

No comments:

Post a Comment