Vilanova hatakuwepo katika benchi la Barcelona
mchezo dhidi ya Cordoba.
Barcelona itaendelea
kuikosa huduma ya kocha wake Tito Vilanova katika mchezo wa kesho wa michuano
ya Copa del Rey katika uwanja wake wa nyumbani dhidi ya Cordoba kufuatia kocha
huyo mwenye umri wa miaka 44 kufanyiwa kipimo cha afya yake hizi zikiwa ni
taarifa ambazo zimethibitishwa na kocha msaidizi Jordi Roura.
Kwasasa kocha
huyo mwenye umri wa atarejea katika benchi baada ya kufanyiwa upasuaji mwezi
disemba lakini nafasi yake itashikiliwa na msaidizi wake katika kipindi hiki wiki
nzima.
Akiongea kocha
msaidizi wake amesema
"Tito hataudhuria
mchezo wa kesho alhamisi kule Camp Nou. Atakuwa akiwa fanyiwa uangalizi wa afya
hivyo hatakuwepo"
Barcelona ilishinda
dhidi ya Cordoba katika mchezo wa kwanza wa mzunguko wa 16 kwa mabao 2-0.
Chama cha soka nchini Korean chawafungia
maisha wachezaji 41 baada ya kuhusika na udanganyifu wa matokeo
Chama cha
soka nchini Korea (KFA) kimewafungia maisha wachezaji 41 kutokana na kutiawa
katika udanganyifu wa matokeo.
Makosa hayo
yalitendeka katika michezo ya ligi ya nchi hiyo K-League mwaka 2011
Bodi ya
utawala ya Fifa nayo kwa upande wake imeongezea rungu la adhabu hiyo kuwa si
nchini Korea peke yake bali ni adhabu ambayo itawagusa wachezaji hao kokote
duniani kiasi kwamba hakuna mchezaji atakaye cheza soka nje ya nchi hiyo.
Beckham anafikiria ofa 12.
David
Beckham kwasasa anajipanga kufanya maamuzi ya hatma yake ya baadaye jumalijalo
baada ya kupokea ofa 12 kutoka sehemu mbalimbali duniani, lakini inaarifiwa
kuwa anafikiria zaidi kumalizia akiwa London.
Kwa mujibu
wa taarifa zilizo zagaa ni kwamba Beckham mwenye umri wa miaka 37, atakuwa na
vikao kadhaa kuelekea katika mustakabali wake wa soka na washauri wake wiki
ijayo.
Mchezaji huyo
wa zamani wa kimataifa wa England ambaye amekuwa hana timu tangu mkataba wake
na Los Angeles Galaxy kumalizika mwezi uliopita, anafikiria ofa mbalimbali
alizo pokea kutoka Ulaya, Marekani ya kusini, Marekani ya Kaskazini, Afrika
kusini, Russia, China na Mshariki ya kati japo si Qatar kama ilivyo fahamika
huko nyuma.
No comments:
Post a Comment