Mlinda mlango wa zamani wa timu ya taifa ya Marekani Kasey Keller akiongea na mwandishi wa TBC Philopo Cyprian wakati ujumbe wa timu ya ligi kuu ya nchini Marekani Seattle Sounders ulipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu JK Nyerere jana jioni. |
Ujumbe wa timu ya Seattle Sounder ya nchini Marekani ukijipanga kuondoka uwanja wa ndege wa Mwalimu JK Nyerere. Katikati ni beki wa timu hiyo Marc Burch( mwenye kofia ya blue) |
Mwenyeji wa ujumbe wa Seattle Sounders Rahim Zamunda Kangezi akijadili jambo na ujumbe wa timu hiyo kabla ya kuondoka uwanja wa ndege kuingia town. |
Marc Burch na Kasey Kessler pamoja na ujumbe wao katika majadiliano. |
Mwandishi wa habari wa TBC Philipo Cyprian katika mahojiano na kiongozi wa ujumbe wa Seattle. |
Bila shaka hii ni zawadi kwa timu ya African Lyon, hapa mkurugenzi wa African Lyon Rahim Zamunda Kangezi akisukuma kwa furaha toroli lenye mipira iliyokuja na ujumbe wa Seattle Sounders. |
Zamunda naye akijibu maswali yanahusu ziara ya Seattle Sounders nchini. |
Mlinda
mlango wa zamani wa klabu za Millwall, Leicester City, Rayo Vallecano,
Tottenham Hotspur, Borussia Moenchengladbach, Southampton, Borussia
Moenchengladbach na Fulham Kasey Keller pamoja na mlinzi wa zamani wa klabu za D.C.
United, L.A. Galaxy na Columbus Crew ambaye kwasasa anachea Seattle Sounders ya
nchini Marekani Marc Burch jana wamewasili nchini kwa ziara ya kitalii ambayo
itaambatana na matukio mengine ya maendeleo ya soka.
Wachezaji
hao ambao wamekuja nchini kama wawakilishi wa klabu ya Seattle Sounders ya
Marekani mbali na mambo mengine wataendesha semina kwa wadau wa michezo hapa
nchini katika ziara yao ya siku tisa kuanzia leo.
Marc Burch ambaye
alisajiliwa na Seattle mwezi Machi mwaka jana akiwa amefuatana na mlinda mlango
mwenye historia ndefu katika soka kabla ya kustaafu na kuanza kazi ya
utangazaji Kasey Keller waliwasili nchini jana jioni wakiwa na ujumbe mzito wa
klabu hiyo kubwa nchini marekani, wakiwa nchini pia wataendesha semina kwa
vilabu vya Ligi Kuu ya Tanzania Bara na shule za msingi katika siku na muda
ambao utangazwa hapo baadaye.
Ziara hiyo
ni moja ya kukuza ushirikiano baina ya Seattle Sounders na wadau wa michezo
nchini.
Ikumbukwe
kuwa timu hiyo iliwahi kumchukua mchezaji nyota wa Tanzania, Mrisho Ngassa
kucheza mechi ya kihistoria dhidi ya timu ya Manchester United.
Kwa
kushirikiana na Washington Global Health Alliance (WGHA), wawakilishi hao
Seattle Sounders, watatembelea miradi mitatu ya upande wa afya iliyopo mkoani
Arusha ikiwa pamoja na World Vision, taasisi ya PATH na Chuo kijulikanacho kwa
jina la Washington State University’s Paul G. Allen School for Global Animal.
Mmiliki wa
klabu hiyo kongwe kabisa nchini Marekani Joe Roth hivi karibuni alitoa taarifa
ya ziara hiyo ya Burch na Keller akisema
”Ziara hii
itadumisha na kuhimarisha uhusiano wetu na serikali ya Tanzania“
Amesema
anatarajia Kesey na Burch watakuwa mabalozi wakubwa wa timu yao katika ziara
hiyo.
Wawakilishi
hao na ujumbe mzima wenye watu zaidi 7 pia utatembelea vivutio vya utalii kama
Ngorongoro Crater na jiji kubwa la Tanzania, Dar es Salaam. Timu hiyo ya
Marekani iliingia katika ushirikiano na WGHA mwaka 2009. Mpango huo una lengo
la kushughulika na masuala ya afya kwa binadamu nchini na Kimataifa.
Keller amekuwa
mlinda mlango namba moja wa timu ya taifa ya Marekani mara nne katika fainali
za kombe la dunia na mmoja wa walinda mlango wa kwanza kuwa namba moja katika
vilabu vya ligi kuu ya nchini England.
Katika miaka
ya 1997,1999 na 2005 alitajwa kuwa mwanamichezo bora wa mwaka ikiwa ni nadra
kupata tuzo kama hiyo mara.
Mzaliwa huyo
wa kitongoji cha Olympia, Keller amecheza zaidi ya mechi katika ngazi ya klabu
na timu ya taifa. Amekuwa mlinda mlango mwenye rekodi kubwa zaidi ya kuidakia
timu ya taifa ya Marekani akidaka michezo 102 na kushinda michezo 53 kati ya
hiyo.
Ameshiriki
kombe la dunia mara nne, ambapo mwaka 1996 alikuwa nahodha wa timu ya taifa ya
nchi hiyo iliyoshiriki michezo ya Olympic.
Alijiunga na
Millwall ya England na kuanza kucheza soka la kulipwa la kueleweka kwa mara ya
kwanza katika ligi ya daraja la kwanza hiyo ilikuwa May 2, 1992 kabla ya
kuelekea Leicester City miaka minne baadaye wakati huo ikishiriki ligi kuu ya
England ‘Premier League’ ambapo mwaka 1997 walishinda taji la ‘League Cup’.
Baada ya
misimu mitatu na Leicester City alijiunga na Rayo Vallecano iliyokuwa
ikishiriki ligi kuu ya Hispania ‘La Liga’. Baadaye alirejea Premier League ambapo
alijunga na Tottenham Hotspur katika misimu miwili ya 2002-03 na 2003-04.
January 15,
2005, Keller alijiunga na Borussia Mönchengladbach ya Ujerumani kabla kuondoka
huko na kurejea kwa mara ya tatu Premier League ambapo alijiunga na klabu ya
jijini London katika viunga vya Craven Cotage na Fulham.
Kwa upande
wake Marc Burch mzaliwa wa Cincinati, Ohio hana historia ya kutisha ambapo
alianzia soka chuo kikuu cha Maryland kabla ya kuelekea D.C. United mwaka 2007
mpaka 2011 na baadaye akajiunga na L.A. Galaxy mwaka 2006 kabla ya kuelekea Columbus
Crew na baadaye mwaka jana akajiunga Seattle Sounders ambayo anaichezea mpaka
sasa.
Huo ndio
ugeni wa kisoka ulioko hapa nchini.
No comments:
Post a Comment