KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, January 10, 2013

HIVI KULIKUWA NA ULAZIMAM GANI SIMBA KUONDOKA NA WACHEZAJI 7 KWENDA OMAN.

Jumla ya wachezaji 8 wa timu ya Simba jana waliondoka iliondoka nchini kwenda kuweka kambi Oman kwa ajili ya mandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania Bara huku wachezaji wake watatu wakishindwa kuondoka kutokana na kukosa visa.

Wachezaji walikosa visa ni Paul Ngalema, Abdallah Juma na Keita, hivyo watawasubiri waondoke januari 13 mwaka huu na wenzao waliobaki na timu Zanzibar.

Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu Bara wameondoka saa tisa ikiwa na wachezaji nane na benchi la ufundi lenye watu wanne.

Waliondoka ni kocha mkuu Mfanransa Leiwing, Kocha msaidizi Basena, Daktari wa timu Cosmas Kapinga na Mtunza vifaa, Kessy.

Wachezaji waliondoka ni mlinda mlango Dhaira, Felex Sunzu, Kigi Makasy, Nassor Masoud "Cholo", Shamte Ally, Ramadhan Chombo na Salum Kinje. 

Wakati timu inaondoka na wachezaji wachache huko Zanzibar walikuwa na wanakabiliwa na jukumu la mchezo wa nusu fainali ngumu dhidi ya Azam fc mchezo ambao kama Simba ingekuwa imedhamiria kufanya kweli basi ni sehemu tosha ya maandalizi yao kucheza ligi na mchezo wao wa kimataifa wa klabu bingwa Afrika.

Bado sijaelewa mantiki ya kuwaondosha wachezaji 8 tu katika mchezo wa nusu fainali ngumu ya kombe la Mapinduzi kwa kisingizio cha kuelekea kuweka kambi ya maandalizi Oman.

Hivi siku mbili hizi za kusubiri kuondoka kwa pamoja mliona mbali sana kiasi kujiondosha kimafungu mafungu mkiwaacha Azam wakiwaondoa vijana wenu kwa penati katika mchezo wa nusu fainali.

Mimi naona hiyo safari ilikuwa ni kuwakoga wafu fulani wasidhani mmeshindwa na safari hiyo kwasababu hata kiongozi wa msafara Saidi Pamba yuko mjini bado sasa nani anawaongozo waliotangulia huko Oman. 

Pamoja na yote hayo bado niwatakie kila kheri katika maandalizi yenu ya huko Oman.

Simba itawakosa wachezaji 6 walioko kwenye timu ya taifa wataungana na wenzao january 12 baada ya mchezo wao na Ethiopia utakaochezwa mjini Adidis ababa januari 11.
Wachezaji hao ni Juma Kaseja, Mrisho Ngassa,Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Shomari Kapombe na Amir Maftah.

Waliobaki Zanzibar kwenye kombe la Mapinduzi kwa ajili ya kumalizia mechi ya nusu fainali ya jana usiku ni Ramadhan Singano, Jonas Mkude, Christopher Edward, Haruni, Seseme, Hassan na Miraji

Pia kiongozi wa msafara Said Pamba ataondoka na wachezaji waliobaki januari 13 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment