Dickson Marwa akimalizia mbio hizo alizofanikiwa kuwa mshindi. |
MWANARIADHA
Dickson Marwa kutoka katika kambi ya Holili, mkoani Kilimanjaro
ameibuka mshindi katika mbio za kilometa 10 za Sokoine Marathon 2013,
zilizofanyika wilayani Monduli, Mkoa wa Arusha kwa kutumia muda wa
dakika 30:42:43.
Dickson
alishinda mbio hizo ikiwa ni takribani wiki moja tu tangu ashinde mbio
za Ngorongoro Marathon zilizofanyika mjini Karatu, na kuwazidi
wanariadha John Leornard wa W.spirit aliyetumia muda wa dakika 30:44:92
na Msenduki Mohammed wa Hakika ya Arusha aliyetumia muda dakika
30:50:05.
Kwa upande wa mbio za wanawake kilometa 10, Catherine Lange wa Magereza Arusha aliibuka mshindi kwa kutumia muda wa dakika 38:17:56, huku akimuacha kwa mbali mshindi wa pili, Fadhila Salum wa JWTZ, aliyemaliza mbio hizo kwa muda wa dakika 38:51:75.
Nafasi ya tatu ilienda kwa Selina Amos, aliyetumia muda wa dakika 39:10:15 huku nafasi za nne na tano zikienda kwa Florah Yudah (41:46:06) na Rosalia Fabiano (41:49:04), wote kutoka JWTZ ya Arusha.
Kwa kuibuka washindi, Dickson Marwa na Cartherine Lange walizawadiwa fedha taslimu shilingi laki moja huku washindi wa pili wakiondoka na shilingi elfu themanini na wa tatu nao wakiondoka na shilingi elfu sitini na cheti kila mmoja.
Lange akizungumza na Waandishi wa Habari muda mfupi baada ya kumaliza mbio hizo. |
Dickson Marwa |
Mbio
za Sokoine Marathon zilikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu za
kifo cha Edward Moringe Sokoine aliyefariki, Aprili 12 mwaka 1984, na
zimefanyikia katika kata ya Monduli Juu, Wilayani Monduli, mkaoni Arusha
na kushirikisha wanariadha zaidi ya 500.
Sokoine Marathon zilihusisha mbio za umbali wa kilometa 2 kukimbia na kutembea kwa watoto na watu wazima VIP na zile za kilometa kilometa 10 kwa wanariadha wazoefu.
Viongozi waliohudhuria Mbio hizo ni pamoja na Waziri
wa Habari, Michezo,Vijana na Utamaduni, Dk. Fenella Mukangala, Mbunge
wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa, Mbunge wa Viti Maalum, Namelok
Sokoine, Mbunge wa jimbo la Arusha mjini, Godbless Lema pamoja na
viongozi wengine akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo.
No comments:
Post a Comment