Ligi
Kuu ya Vodacom inaendelea tena hii leo Aprili 13 kwa mechi mbili
zitakazochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, na Uwanja wa Kumbukumbu
ya Sokoine jijini Mbeya.
Yanga
itakuwa mwenyeji wa Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa wakati Uwanja wa
Sokoine utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Tanzania Prisons na Ruvu
Shooting.
Ligi
hiyo itaendelea kesho Aprili 14 kwa mechi kati ya
wenyeji Azam na Simba. Mechi hiyo namba 155 itachezwa kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment