KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, May 27, 2013

John Mikel Obi sasa kuichezea Nigeria michuano ya mabara, Torres aitwa timu ya taifa ya Hispania, Lazio yatwaa taji la Copa Italia na Cristal Palace yapanda daraja. Soma.....................



Kiungo wa Chelsea John Mikel Obi amethibitisha kujiunga na kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria kuelekea katika michezo ya kufuzu kombe la dunia na kichuano ya kombe  la shirikisho nchini Brazil.
Mikel alikuwa katika mashaka makubwa kufuatia kuwa katika majukumu na klabu yake lakini pia kutokana na tatizo la visa.
Shirikisho la soka la nchini Nigeria (NFF) limetanabaisha kuwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26 hatakuwepo katika mchezo wa kimataifa wa kirafikia dhidi ya Mexico May 31.
Hata hivyo shirikisho hilo limethibitisha kuwa atapatikana katika michezo miwili dhidi ya Kenya na Namibia, pamoja na michezo ya michuano  ya shirikisho yaani Confederations Cup.
Kueleka katika michezo yao ya hivi karibu mwezi wa juni mabingwa hao wa soka barani Afrika watakuwa wakiwakosa wachezaji wao wakali wakiwemo majeruhi Victor Moses, Kalu Uche na Gabriel Rueben.
Watamkosa pia mfungaji bora wa fainali za mataifa ya Afrika Emmanuel Emenike, ambaye anasumbuliwa na mguu.
Super Eagles wako sawa kwa alama na Malawi katika kundia F la kuwania kufuzu kombe la dunia wakiwa wote wana alama tano wakati ambapo kiongozi wa kundi akitarajiwa kusonga mbele katika changamoto nyingine ya kusaka nafasi ya kufuzu.

Baada ya kufunga bao europa league Fernando Torres aitwa kikosini Hispania kucheza kombe la mabara
Mshambuliaji aliyekuwa hapewi nafasi ya kuwemo katika kikosi cha timu ya taifa kutoka na kiwango chake kutoridhisha Fernando Torres ametajwa na Hispania kujiunga katika kikosi cha timu ya taifa kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya kombe la shirikisho la mabara.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka , 29, ambaye akiwa na klabu yake alifanikiwa kutwa taji la Europa League msimu huu hivi karibuni alishindwa kumshawishi kocha Vicente del Bosque katika kikosi chake.
Wengine wanane wanaocheza cheza soka nchini England wameitwa ambapo baadaye kikosi hicho kitapunguzwa kutoka jumla ya wachezaji 26 na kusaliwa na wachezaji 23 kabla ya kuaanza kwa michuano hiyo nchini Brazil june 15.
Mlinzi wa Barcelona Carles Puyol na mshambuliaji wa  Sevilla Alvaro Negredo wameachwa na kocha huyo.
Mlinda mlango wa Real Madrid na nahodha wa Hispania aliyevunjika kidole mwezi Januari Iker Casillas wamerudishwa huku kiungo Javi Martinez aliye katika kiwango safi akiwa na Bayern Munich ambao wametwaa taji la Champions League wote wameitwa.
Torres alikuwa na msimu mzuri akiwa na Chelsea akifunga jumla ya magoli 22 baada ya kucheza michezo 64 ikiwa ni pamoja na kufunga goli la kwanza katika mchezo wa ushindi wa mabao 2-1 wa fainali ya Europa dhidi ya Benfica.
Goalkeepers: Iker Casillas (Real Madrid), Jose Reina (Liverpool), Victor Valdes (Barcelona).
Defenders: Jordi Alba (Barcelona), Raul Albiol (Real Madrid), Alvaro Arbeloa (Real Madrid), Cesar Azpilicueta (Chelsea), Nacho Monreal (Arsenal), Gerard Pique (Barcelona), Sergio Ramos (Real Madrid).
Midfielders: Xabi Alonso (Real Madrid), Benat Etxebarria (Real Betis), Sergio Busquets (Barcelona), Santi Cazorla (Arsenal), Cesc Fabregas (Barcelona), Javi Garcia (Manchester City), Andres Iniesta (Barcelona), Javi Martinez (Bayern Munich), Juan Mata (Chelsea), Jesus Navas (Sevilla), Pedro (Barcelona), David Silva (Manchester City) Xavi (Barcelona).
Forwards: Fernando Torres (Chelsea), Roberto Soldado (Valencia), David Villa (Barcelona).

Lazio yatwaa Coppa Italia baada ya kuwafunga Roma katika fainali
Lazio imeshinda taji la Coppa Italia kwa mara ya sita baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wapinzani wao wakubwa Roma mchezo uliopigwa Stadio Olimpico.
Senad Lulic alifunga bao pekee la ushindi kwa mabingwa hao kufuatia mlinda mlango wa Roma Bogdan Lobont kushindwa kuifuata krosi ya Antonio Candreva.

Nafasi kubwa ya Roma kusawazisha ilikuwa pale mpira wa adhabu ya moja kwa moja uliopigwa na mkongwe Francesco Totti kugonga mtamba wa panya.
Ushindi wa Victory Lazio, ambao walimaliza msimu katika nafasi ya saba katika ligi kuu ya Italia Serie A, unamaanisha kuwa watakuwa wamefuzu moja kwa moja kucheza Europa League hatua ya makundi.
Lazio imeshinda mara nne katika mara tano walizokutana na wapinzani wao wakubwa hao huku matokeo mengine yakiwa ni sare ya 1-1 mwezi April.

CRISTAL PALACE YAPANDA DARAJA
Mkongwe Kevin Phillips hii leo ameifungia goli muhimu kwa Crystal Palace iliyokuwa bora na iliyostahili kuichapa Watford katika mchezo wa fainali wa Championship play-off uliopigwa katika dimba la Wembley.

Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 39 alifunga goli hilo kwa mkwaju wa penati katika dakika za majeruhi za kipindi cha kwanza na kumaliza kiu ya kusubiri kwa miaka nane kupanda daraja na kucheza ligi kuu ya soka nchini England Premier League.

Ilkuwa ni penati nzuri iliyotokana na mlinzi Marco Cassetti wa Watford kumfanyia madhambi mshambuliaji mtarajiwa wa Manchester United Wilfried Zaha, ambaye amekuwa katika kikosi cha Palace tangu akiwa na umri wa miaka tisa na akicheza mchezo wa fainali kabla ya kuelekea kwa Manchester United wakati wa kipindi cha uhamisho cha majira ya kiangazi.

Ushindi huo unawafanya Crystal Palace kuungana sasa na kikosi cha meneja Ian Holloway cha Blackpool kucheza ligi hiyo.

Palace ilikuwa kidogo ishuke daraja katika msimu wa 2009-10 huku ikiwa katika uangalizi tangu iliposhuka daraja lakini kwasasa inatazama mbele kuweka historia nyingine.

No comments:

Post a Comment