KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, June 13, 2013

Cesc Fabregas atoa nje ofa yoyote ya kuondoka Barcelona na kuelekea England

Kiungo wa Barcelona Cesc Fabregas amekanusha taarifa kuwa anataka kurejea kwa kusema haina mana na kichekesho.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26 alijiunga Barcelona msimu wa 2011 lakini Manchester United na klabu yake ya zamani Arsenal zinaamini kuwa zinaweza kumng'oa Nou Camp.
Amenukuliwa kiungo huyo akisema:
"Mara zote nimekuwa nikisema ninafuraha ndani ya klabu ya Barca. Yeyote anaesema kuwa ninaondoka, huyo hanijui vizuri na hajawahi kuongea na mimi ".
"Kama kuna mtu anasema sitaki kuchezea Barca, ni wazi kabisa kuwa hana maana." 
Fabregas ameibuka na kulelewa katika kituo cha vijana cha Barcelona alipoanzia akiwa na umri wa miaka 10 mpaka 16, kabla ya kujiunga na washika mitutu wa London Arsenal.
Aliichezea Asernal jumla ya michezo 303 ndani ya kipindi cha miaka minane akifunga jumla ya magoli 57 ambapo alikuwa mchezaji mdogo kuitumikia klabu klabu hiyo katika mchezo dhidi ya Rotherham United akiwa na umri wa miaka 16.

No comments:

Post a Comment