Timu ya Anzhi
Makhachkala ya Urusi imeliandikia barua shirikisho la soka la Cameroon kutaka
nchi hiyo isimtumie Samuel Eto'o katika michezo ijayo ya kampeni ya kuwania
kufuzu kombe la dunia mwaka 2014.
Mtaalamu wa
mambo ya tiba za viungo wa klabu hiyo physiotherapist, Stijn Vandenbroucke, amesema
mshambuliaji huyo yuko katika maumivu ya msuli aliyoyapata katika mchezo wa
fainali ya Russian Cup.
Katika taarifa
yao wamesema mshambuliaji huyo anatakiwa kupumzika kwa wiki chache.
Eto'o anatarajiwa
kuwasili nchini Cameroon hii leo ili kwamba timu ya waangalizi wa afya ya Indomitable
Lion nayo iweze kumfanyia uchunguzi.
Hata hivyo
daktari wa timu ya Cameroon ndiye mwenye kauli ya mwisho ya kuamua kama Eto'o yuko
fiti ama laa na kama ataweza kutumika katika mchezo wa june 9 dhidi ya Togo na
mchezo mwingine dhidi ya DR Congo wiko moja baadaye.
Cameroon wanaongoza
kungi I wakiwa na alama sita ikiwa mbele kwa alama moja dhidi ya Libya huku DR
Congo ikiwa na lama nne na Togo ikiwa na alama moja.
St George imekuwa timu ya kwanza
kutoka Ethiopian kutinga hatua ya makundi ya michunano ya kombe la shirikisho
St George imefanikiwa
kuwa timu ya kwanza kutoka Ethiopian kufuzu kwa hatua ya makundi ya kombe la
shirikisho barani Afrika licha ya hapo jana kupata kichapo kutoka kwa ENPPI ya
Misri.
ENPPI ilishinda
katika mchezo huo wa mkondo wa pili wa kwa bao 3-1 matokeo ambayo yalifanya
matokeo ya jumla kusimama kuwa sare ya 3-3 lakini timu hiyo ya Ethiopian imefanikiwa
kusonga mbele kwa faida ya sheria ya kupata bao la ugenini.
St George itaungana
na Stade Malien ya Mali, Enugu Rangers ya Nigeria na Etoile du Sahel ya Tunisia
katika kundi A la michuano hiyo.
Mabingwa wa Algerian
Entente Setif, TP Mazembe ya DR Congo, FUS Rabat ya Morocco na CA Bizertin ya
Tunisia zote zilipata ushindi katika michezo yao na sasa zinajumuika katika kundi
B.
Mshambuliaji
raia wa Ivory Coast Vincent Die Foneye alifunga bao la uongozi kwa wenyeji ENPPI
baada ya dakika 25 za mchezo lakini Tesfaye Alebachew aliwapa wenyeji wakati
mgumu kufuatia kusawazisha bao hilo dakika 12 baadaye.
Die Foneye kwa
mara nyingine tena akaandika mabao yake mawili kwa kwa ENPPI katika dakika sita
za mwisho na kundika “hat-trick” lakini haikufua dafu hivyo St George ikafuzu.
Stade Malien
imeichapa Lydia LB Academic ya Burundi kwa bao 1-0 na kuandika ushindi wa jumla
wa mabao 6-0.
Mabingwa mara
mbili wa zamani CS Sfaxien wameondolewa mashindanoni kufuatia sare ya bila
kufungana na Enugu Rangers ya Nigeria ambao wamepita kwa ushindi wa jumla wa
bao 1-0.
FUS Rabat
wenyewe wamefanikiwa kusonga mbele baada ya sare ya mabao 3-3 wa Rabat derby dhidi
ya FAR Rabat hapo jana na hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-3.
Mchezaji wa
zamani wa Hibernian Abdesselam Benjelloun aliwapa FUS bao la uongozi dakika
tatu yan mchezo kabla ya Mustapha El Yousfi kusawazisha dakika 30 baadaye.
FAR wakaandika
bao linguine la pili kupitia kwa Mustapha Allaoui kunako dakika ya 60 lakini
mabao mawili ndani ya dakika tatu kupitia kwa Hicham Laroui na Benjelloun yakawapa
uongozi FUS tena.
Hata hivyo
dakika ya mwisho Youne
ss Hammal akaandika bao la kusawazisha kwa wanajeshi hao
na kusonga mbele.
Kulikuwa na
taarifa mbaya kwa waarabu wengine wa Misri Ismaili ambao wametolewa mashindano
licha ya ushindi wa nyumbani wa bao 1-0 dhidi ya CA Bizertin Tunisia.
Watunisia hao
wamesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabaoa 3-1 baada ya ushindi wa mchezo
wa kwanza wa mabao 3-0.
TP Mazembe ya
DR Congo, chini ya Patrice Carteron pia imesonga mbele licha ya kichapo cha mabao 2-1 toka kwa Liga
Muculmana ya Mozambique.
No comments:
Post a Comment