Leighton Baines |
Klabu ya Everton, imekata ombi
lililowasilishwa na Manchester United la kutaka kumsajili mlinda lango
wake Leighton Baines kwa kitita cha pauni milioni kumi na mbili.
Kocha mpya wa Manchester David Moyes ambaye
alisajiliwa hivi majuzi kutoka kwa klabu hiyo ya Everton alitaka
kumasjili mchezaji huyo ili kuimarisha safu yake ya ulinzi.
Siku
chache tu baada ya kusajiliwa kama kocha wa Manchester United Moyes,
alitangaza wazi wazi kuwa nia yake kuu ni kumsajili mechaji huyo mwenye
umri wa miaka ishirini na minane.
Ripoti zinasema Manchester United inajianda kuwasilisha ombi lingine baada ya kuongeza fedha za kumsajili.
Hata hivyo, wasimamizi wa Everton, wamesema kuwa hawana nia yoyote ya kumuuza mchezaji huyo.
Kocha mpya wa Everton, Roberto Martinez kwa
upande wake amesema anataka mchezaji huyo ambaye aliteuliwa kuwa
mchezaji bora wa mwaka msimu uliopita kusaini mkataba mpya.
Uamuzi huo wa Moyes wa kutaka kumsajili, Baines,
huenda ukahujumu nafasi ya mcheza kiungo wa Manchester United Patrice
Evra mwenye umri wa miaka thelathini na miwili.
No comments:
Post a Comment