Roger Palmgren ameamua kuachana na
kazi ya kuifundisha timu ya taifa ya Namibia kufuatia yeye na familia yake
kupokea vitisho vya kuuwawa.
Rais wa shirikisho la soka la Namibia
John Muinjo amesema "Roger ametutumia ujumbe wa barua pepe akisema amesema
maisha yake yake kwenye vitisho na kwa msingi huo ameamua kujiuzulu"
“Nimekuwa katika soka kwa muda mrefu
nimeshudia makocha wakiajiriwa na kufukuzwa lakini sikuwahi kushuhudia hili
likitokea”
"Roger hakushirikiana na sisi
kuhusi jambo hili hivyo hatukuweza kulishughulikia kujua ni nani anahusika,
hatukuwa na mazungumzo naye".
"Htukuwahi kuwa na tatizo hilo
huko nyuma ninaogopa endapo itakuwa kweli. Sina hakika kwa asilimia 100% kama
ni kweli, Itakuwa vizuri kama tungelifanyia uchunguzi"
Kujiuzulu kwa kocha huyo raia wa Sweden
kunafuatia masaa 48 kabla ya timu ya taifa ya Namibia maarufu kama 'Brave
Warriors' haijawakaribisha vinara wa kundi F Nigeria katika mchezo ambao kwao
ni lazima kushinda ili kuwepa veam kampeni ya kufuzu kucheza kombe la dunia 2014.
Namibia inahitaji kujikusanyia zaidi
alama ili kuweka hai matumaini yao ya kufuzu wakiwa na nafasi finyu ya kuingia
katika timu za mwisho zitakazo cheza michezo ya mtoano yaani play-off round kuamua watakao fuzu
fainali za nchini Brazil mwakani.
Kocha huyo wa zamani wa Sierra Leone
na Rwanda Palmgren, mwenye umri wa miaka 50, alichukua nafasi hiyo mwezi
uliopita na mchezo wake wa kwanza wa kimashindano ulikuwa nchini Malawi ambapo
walikwenda sare 0-0 na wenyeji wao katika kampeni ya kufuzu kombe la dunia.
Kocha msaidizi Ricardo Mannetti na Ronnie
Kanalelo wanachukua nafasi ya kukinoa kikosi cha Namibia kuelekea katika mchezo
dhidi ya Nigeria.
No comments:
Post a Comment