Robin Van Persie akifanya mazoezi na kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi kuelekea katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya China mjini Beijing |
Robin van Persie amepokea vizuri zama mpya ya klabu ya Manchester United lakini ameomuonya bosi mpya wa klabu hiyo David Moyes kuwa hakuna cha zaidi isikuwa ni kulinda na kutetea taji la ligi kuu Premier League.
Moyes
alichukua nafasi ya m-Scotishi mwenzake Sir Alex Ferguson katika badiliko la kwanza la klabu hiyo la uongozi ndani ya robo karne.
Hata hivyo Van Persie, mbaye alitwaa taji lake la kwanza la ligi katika mwaka wake wa kwanza ndani ya klabu hiyo ana matumaini kuwa itakuwa ni biashara kubwa linapokuja suala la kushinda mataji.
Moyes atakuwa katika shinikizo kubwa la kutwaa mataji katika kikosi cha baada ya kujiunga na klabu hiyo akitokea Everton
Amenukuliwa na MUTV mshambuliaji huyo akisema
'Itakuwa ni zama mpya na tunaangalia mbele, sehemu ya kazi yetu pia. Tunapaswa kupambana na hali hiyo mpya na ndivyo ilivyo'.
United
itakuwa ikipambana na upinzani mkubwa kutoka katika vilabu vya Chelsea na wapinzani wao wa jiji la Manchester, Manchester
City vilabu ambavyo vimebadilisha maisha kwa kuchukua mameneja wapya'.
Wilfried Zaha (kulia) anatarajiwa kujiunga na United.
No comments:
Post a Comment