Mfungaji bora
wa muda wote wa Afrika kusini Benni McCarthy amestaafu soka rasmi akiwa naumri
wa miaka 35.
McCarthy alikuwa
akiichezea Orlando Pirates tangu mwaka 2011 alipoihama West Ham.
Amekaririwa akisema
"Soka
lilikuwa zuri kwangu – limenipa wakati mzuri na kuniwezesha kuwa katika nafasi nzuri
ya kuimarisha maisha yangu.
"kwa
hilo najivunia."
Vilabu alivyopitia Benni McCarthy
Orlando Pirates (S Africa)
West Ham (England)
Blackburn Rovers (England)
FC Porto (Portugal)
Celta Vigo (Spain)
Ajax Amsterdam (Netherlands)
Cape Town Spurs (S Africa)
Seven Stars (S Africa).
Mzaliwa huyo
wa Cape Town alikuwa akichezea ligi kuu ya Uholanzi, Hispania, Ureno na England,
na kushinda taji la Eredivisie akiwa na Ajax na taji laligi ya Ureno mwaka 2004
akiwa na Porto ya Ureno wakati huo ikiwa chini ya Jose Mourinho.
Ameendelea kunukuliwa
akisema
"Nimebarikiwa
kufurahia kazi ya soka ambayo kutoka katika soka la mchangani vya viwanja vya Nyanga
mpaka kushinda medali katika Uefa Champions League na kombe la dunia la vilabu –
kiwango cha juu ambacho mchezaji anaweza kufanikisha katika soka la ngazi ya
vilabu".
Amestaafu kama
mfungaji bora wa kihistoria katika soka la kimataifa akifunga magoli 31 baada
ya kushuka uwanjani mara 80.
Licha ya
kuachwa katika timu ya taifa ya wakati timu ya taifa ilipokuwa wenyeji wa
fainali ya kombe la dunia mwaka 2010, McCarthy aliifungia timu ya taifa ya nchi
hiyo maarufu kama Bafana Bafana katika fainali za mwaka 1998 na 2002.
Alirejea Afrika
kusini baada ya kuvitumikia vilabu vya Blackburn na West Ham nchini England kabla ya
kujiunga na vijana wa kitongoji cha Soweto, Orlando Pirates mwaka 2011.
Ameshinda taji
akiwa na Pirates mwaka 2012.
Aston Villa kuwaacha Richard Dunne, Eric
Lichaj na Andy Marshall.
Mlinzi wa
kimataifa wa jamhuri ya Ireland Richard Dunne ni miongini mwa wachezaji watatu
watakao achwa na Aston Villa.
Mlinzi huyo
mwenye umri wa miaka 33 ameichezea Villa jumla ya michezo 111 tangu kujiunga
nayo mwaka 2009 akitokea katika klabu ya Manchester City kwa uhamisho wa pauni
milioni £5 mwezi September 2009.
Mlinzi wa
pembeni Eric Lichaj mwenye umri wa miaka 24, na mlinda mlango Andy Marshall,mwenye
umri wa miaka 38, nao pia wataondoka pamoja na Dunne, ilhali mlinzi Jean Makoun na
mshambuliaji Simon Dawkins pia wakitarajiwa kuondoka.
Makoun
mwenye umri wa miaka 30, anaelekea kujunga na Rennes ya Ufaransa kwa mkopo huku
Dawkins, 25 akirejea Tottenham.
Dunne
amemaliza msimu huu akiwa na matatizo ya msuli maumivu aliyoyapata katika
mchezo aliocheza kwa dakika 25 dhidi ya Georgia mjini Dublin jumapili iliyopita.
Nyota wa
kimataifa wa Cameroon Makoun, ambaye alijunga na Villa akitokea Lyon kwa ada ya
pauni milioni £6 mwaka 2011, anarejea Ufaransa katika klabu ya Rennes alikochezea
kwa mkopo.
Dawkins ambaye
aliichezea Villa michezo minne baada ya kujunga nayo akitokea Spurs kwa mkopo
mwezi January, ilhali mmarekani Lichaj akiichezea michezo 23 kikosi cha Paul
Lambert msimu huu.
Bayern Munich yamuongezea mkataba Franck Ribery miaka miwili.
Winga wa Bayern
Munich Franck Ribery amesaini kuongeza mkataba wa miaka miwili na klabu yake
hiyo ambao ni mabingwa wa vilabu Ulaya mkataba ambao utamuweka hapo mpaka 2017.
Mfaransa huyo
mwenye umri wa miaka , 30 aliisaidia Munich kuwa timu yan kwanza ya Ujerumani
kushinda kwa pamoja mataji matatu ndani ya msimu mmoja yakiwemo mataji ya Bundesliga,
European Cup na German Cup.
Mlinzi raia
wa Belgiam Daniel Van Buyten mwenye umri wa miaka 35, naye anatarajiwa kusalia
hapo kwa mwaka mmoja zaidi.
Bayern ndiyo
timu ya kwanza nchini Ujrumani kutwa
mataji mengi yakiwemo ya ligi ya nyumbani na Ulaya ndani msimu mmoja.
Inakuwa ni
timu ya saba kufanya hivyo barani Ulaya kama ilivyokuwa kwa Celtic mwaka 1967,
Ajax mwaka 1972, PSV Eindhoven mwaka 1988, Manchester United mwaka 1999,
Barcelona mwaka 2009 na Inter Milan mwaka 2010.
Arsene Wenger kuongezewa mkataba mwingine anasema mtendaji mkuu Ivan Gazidis
Mtendaji mkuu wa Arsenal Ivan Gazidis anaamini kuwa meneja wao Arsene Wenger ataendelea kusalia kwa muhula mwingine.
Wenger
mwenye umri wa miaka 63, anaanza msimu mpya ambao unakuwa ni wa mwisho ndani ya
mkataba wake huku Arsenal wakitegemea kumpa mkataba mwingine.
Historia ya Wenger ndani ya Arsenal kwa kipindi chote
2012-13: League - 4th; Champions League -
last 16; FA Cup - 5th round; League Cup - 5th round
2011-12: League - 3rd; Champions League -
last 16; FA Cup - 5th round; League Cup - 5th round
2010-11: League - 4th; Champions League -
last 16; FA Cup - quarter-finalists; League Cup - finalists
2009-10: League - 3rd: Champions League -
quarter-finalists; FA Cup - 4th round; League Cup - 5th round
2008-09: League - 4th; Champions League -
semi-finalists; FA Cup - semi-finalists; League Cup - fifth round
2007-08: League - 3rd; Champions League -
quarter-finalists; FA Cup - 5th round; League Cup - semi-finalists
2006-07: League - 4th; Champions League -
last 16; FA Cup - 5th round; League Cup - runners-up
2005-06: League - 4th; Champions League -
runners-up; FA Cup - 4th round; League Cup - semi-finalists
2004-05: League - 2nd; Champions League -
last 16; FA Cup - winners; League Cup - 5th round
Amekaririwa Gazidis akisema
"Tumepata
meneja safi. Tuna matumaini ya kuwa anataka kufanya kile anachokifanya kwa muda
mrefu. Tuna amini anafanya hivyo.
"Kimya
kimya na kwa wakati muafaka tutatangaza mpango wake mpya mara baada ya mambo kuwa
mwenye nafasi"
Tottenham yamtaja Franco Baldini kuwa mkurugenzi wa ufundi.
Tottenham inajipanga
meneja wa zamani wa England assistant Franco Baldini kuwa mkurugenzi wake wa
ufundi.
Mtaliano huyo
mwenye umri wa miaka , 52, aliachia nafasi hiyo katika klabu ya Roma jumatano
na atachukua nafasi katika klabu ya Spurs katika kazi ya kusimamia usajili na
sera za uhamisho.
No comments:
Post a Comment