Bei ya Tiketi za kutizama mechi za ligi kuu ya Uingereza zimeshuka kwa asilimia 2.4 kulingana na utafiti wa kitengo
cha michezo cha BBC.
Utafiti huu uliojumuisha vilabu 166 kutoka
kwenye daraja kumi bora nchini Uingereza,Imebaini kuwa kati ya msimu wa
2013 - 2014 bei ya kiingilio ya mechi ilishuka katika daraja nne za juu
katika ligi ya Uingereza.
'' Hii ni Habari njema kwa mashabiki
wa Kandanda ambao wamekuwa wakistahimili kupanda kwa bei mwaka nenda
mwaka rudi '' Waziri wa michezo wa Uingereza Hugh Robertson aliiambia
BBC.
''Vilabu vimebaini kuwa bei ya tiketi za
kutizama mechi zimepanda kwa asilimia 11 ambayo ilikuwa ni mara nne ya
kiwango cha mfumuko wa bei ya bidhaa asili.
Hilo limelazimu vilabu vianze kujali maslahi ya mashabiki wake kwa kupunguza bei.
Aidha idadi ya mashabiki wanaofika Viwanjani
imeshuka kwa asili mia 5% ikiashiria mashabiki 9949 katika msimu wa
mwaka wa 2011 -2012 hadi mashabiki 9481 katika msimu wa 2012-2013.
Mashabiki walilazimika kutoa takriban pauni
336.23 kutizama mechi zote katika msimu asilimia 2.4 chini ya msimu
uliokwisha ambapo tikiti za msimu ziligharimu pauni 344.63 .
Tiketi ghali zaidi katika ligi ya premia ni ile
ya Arsenal ambayo inagharimu pauni 126 katika eneo maalum na pauni 26
katika maeneo ya kawaida.
Aidha tikiti nafuu zaidi ya msimu ni ile ya
Manchester City ambayo inauzwa kwa pauni 299 pekee huku ile ya Arsenal
ikiorodheshwa kuwa ghali mno ikiuzwa kwa pauni 1,955.
Na ukitaka kikombe cha chai kuwa tayari kutoa pauni 2.50 ukiwa old Trafford nyumbani kwa Manchester United.
No comments:
Post a Comment