Cristiano Ronaldo amekiandikia kituo cha polisi cha Miami ombi la kutaka kuondoa shitaka dhidi ya shabiki wa mpiwa kijana aliyeingia ndani ya uwanja na kumkumbatia (huggy) wakati wa michezo ya maandalizi ya msimu.
Ronald Gjorka, mwenye umri wa miaka 20 ambaye ni shabiki wa kupindikia wa Real Madrid alirukia ndani ya uwanja wakati wa mchezo dhidi ya Chelsea huko Marekani na moja kwa moja kumvaa na kumkumbatia nyota Ronaldo kwa muda.
Tukio hilo lilichukua muda mrefu mpaka polisi walipo fanikiwa kuingia ndani ya uwanja na kuwaachanisha Gjorka na Ronaldo kabla ya kumtia kizuizini shabiki huo na kufunguliwa mashitaka.
Wakati kijana huyo akiwa sasa katika hatua ya kumuondoa chuoni anakosoma na kurejeshwa kwao nchini Albania endapo atakutwa na hatia, tayari Ronaldo ameingilia kati na kumsaidi kijana huyo.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureno ameandika barua kwenda kwenye mamlaka wiki hii akitaka waachane na shauri hilo dhidi ya Gjorka, na kumruhusu aendelee kusalia nchini Marekani.
Amenukuliwa akisema,
‘Naelewa nafasi yako na umuhimu wa sheria’.
‘Hata hivyo, kwa heshima na taadhima ningeomba wewe na ofizi yako kufikiria mara ya pili maamuzi ya hilo na kuachana na kesi hiyo.’
Bado haijawekwa wazi endapo nguvu ya ombi la barua hiyo itafua dafu lakini Ronaldo.
No comments:
Post a Comment