Wakati dirisha dogo la usajili nchini England likiwa linaelekea kufunguliwa na huku wakuu wa vilabu mbalimbali wakiwa na malengo mbalimbali ya kufanyia mabadiliko vikosi vyao, kwa upande wa Manchester United mambo yanaonekana kuwa ni zaidi ya biashara hususani kwa wachezaji wenye majina makubwa zaidi.
Baada ya kuwakosa wachezaji kadhaa David Moyes kwa hakika atakuwa akitaka kuboresha kikosi chake mwezi ujao wa Januari.
Bosi huyo mpya atakuwa akisaka wachezaji watakao kuwa na uwezo wa kusababisha mashambulizi kutokea eneo la kati wakati usajili wa kipindi cha kiangazi wa kiungo Marouane Fellaini ukionekana kuendelea kutokuzaa matunda.
What do they need?
United imekuwa ikisaka wachezaji kote duniani ‘world-class
players' karibu katika kila eneo ikiwa ni jitihada za kuweka kikosi katika ubora zaidi.
Kwa muda mrefu United imekuwa ikihitaji damu mpya sehemu ya kiungo, huku wakiendelea kuwa hovyo uwanjani.
Sir Alex Ferguson alikuwa akijua hili wakati akielekea kustaafu ingawa hakuwa tayari kulisema, haijulikani ni biashara ya aina gani United watakwendakufanya mwezi Januari hilo ndilo linalosubiriwa kwa hamu.

David Moyes hatakiwi kufanya makosa mwezi Januari kuimarisha kikosi cha Manchester United chenye soka mbovu kwa hivi sasa.

Andres Iniesta (kulia) hataki kuondoka Barcelona licha ya United kuendelea kuonyeshania.

Marouane Fellaini amekuwa akijitahidi kuonyesha mabadiliko ndani ya kikosi tangu ajiunge kiangazi lakini wapi.
Nani kuingia nani kutoka januari United?
Wakati wa kiangazi iliyopita United
ilishindwa katika jaribio lake la kumtaka kwa mara nyingine Cristiano Ronaldo kurejea Old Trafford kabla ya Mreno huyo kuongeza mkataba ndani ya Real Madrid, na huo ungekuwa ni usajili wa kichwa cha habari kikubwa ambao wangependa kuufanya.
Garreth Bale alikuwa ni mmoja wa wachezaji walioshindwa kujiunga na kikosi cha David Moyes ambaye bado mpaka sasa anataka kwa udi na uvumba saini ya kiungo Andres Iniesta
na wenzake wawili kutoka Barcelona Cesc Fabregas na Alex Song, pamoja na Luka Modric wa Real Madrid.
Moyes
pia anaonekana kuvutiwa na mshambuliaji wa Borussia Dortmund Marco Reus huku swali likiwa bado juu ya mustakabali wa Robie van Persie kusalia Old Trafford kama ilivyo kwa Wayne Rooney na Javier Hernandez kutokana na kuibuka kwa mara kwa mara sababu za matishio ya kutaka kuondoka.
Herrera
anaendelea kusalia katika rada ya United tangu alipopoteza kiwango chake ndani ya Bilbao huku pia United wakiendelea kumfukuzia mshambuliaji wa Roma aliyethaminishwa kwa pauni milioni £30 pamoja na Ilkay Gundogan wa Dotmund.
Mawindo ya meneja wa zamani wa United Sir Alex Ferguson ya kiungo Wesley Sneijder, ni changuo lingine lakini ugumu unakuja kutokana na umri wa nyota huyo wa Galatasaray ambaye kwasasa ana umri wa miaka 29.

Nyota wa Borussia Dortmund Marco Reus (kushoto) huenda akajiunga na United Januari.


Viungo Wesley Sneijder (kushoto) na Cesc Fabregas mawindoni United
Nyota wa Montpellier Remy Cabella huenda akatua United Januari pamoja na kiungo mwingine wa Everton Ribeiro Cruzeiro, Koke (Atletico Madrid) na Yohan Cabaye (Newcastle) pamoja na William Carvalho (Sporting Lisbon) licha ya kwamba orodha imekuwa ikiongezeaka kila wakati.
Mlinzi wa kushoto Patrice Evra anakaribia kufikia umri wa 33rd na kuna wasiwasi juu ya Alex Buttner na Fabio kuchukua nafasi yake moja kwa moja.
Wasaka wachezajin wa United wanahaha kupata huduma ya Alex Sandro wa Porto na mlinzi wa St Etienne Faouzi Ghoulam.
Kuna hali ya wasiwasi katika eneo la ulinzi wa kati ambapo Rio Ferdinand na Nemanja
Vidic wanaelekea ukingoni wa kucheza soka la ushindani wakisaidiwa zaidi na vijana Jonny Evans
na Chris Smalling au Phil Jones katika partnership ya kikosi cha kwanza.
Cristian Zapata wa AC Milan yuko katika orodha ndefu ya wanao waniwa na United.

Ander Herrera windo lingine la United kutoka Athletic Bilbao
Nani wa kuondoka?
Kama United inataka kuziba mapengo huenda Anderson akawa wa kwanza kuonyeshwa mlango wa kutokea. Ashley Young pia anaonekana kuisha huku meneja Moyes akionekana kuvutiwa na Adnan
Januzaj na Wilfried Zaha.


Wanting out? Robin van Persie inaelezwa kuwa si mwenye furaha United
Best ever January buy?
Cantona
aliwasili Novemba ambapo pia mwaka 2006 alisajiliwa Nemanja Vidic na Patrice Evra in the 2006 pamoja na Andy Cole 1995.
January signing to forget?
Wengine ambao wameshasahaulika ni pamoja na Diego Forlan kwa £6.9 mwaka 2002,
Manucho mwaka 2008 na Ritchie De Laet mwka 2009

Wilfried Zaha anatakiwa na vilabu vingi vya Premier League kwamkopo.
No comments:
Post a Comment