KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, December 16, 2013

Sergio Aguero nje ya uwanja mwezi mzima

Sergio Aguero atakuwa nje ya uwanja kwa takribani mwezi mzima hizi zikiwa ni taarifa zilizothibitishwa na bosi wa Manchester City Manuel Pellegrini.

Mshambuliaji huyo wa City alipatwa na maswahibu ya maumivu ya msuli katika mchezo wa ushindi mnono wa mabao 6-3 Jumamosi dhidi ya Arsenal ambao ndio vinara wa ligi kuu ya England.

Muajentina huyo mwenye mabao 13 ya ligi alifunga bao la uongozi la Gunners kabla ya kutoka mapema kipindi cha pili.

Pellegrini amethibitisha hilo leo mbele ya wanahabari.

City inajipanga kucheza dhidi ya Leicester City katika mchezo wa robo fainali ya League Cup hapo kesho.

No comments:

Post a Comment