![]() |
Partick Thistle huenda ikawa ni klabu ambayo inapokuwa uwanjani haina la kushangaza lakini huku nyuma ya pazia inapokuwa katika uwanja wake wa mazoezi vituko ni sehemu ya kufurahisha ndani ya klabu hiyo ya Uskochi.
Kiungo Gary Fraser mwenye umri wa miaka 19 akiwa mazoezini alivalia kivazi cha kufungia mwaka cha rangi ya pinki ambacho kimeunganishwa na sketi iliyokuwa katika rangi moja.

Fraser kwasasa yuko kwa mkopo katika klabu ya Bolton Wandarers ya Uskochi.
Inadhaniwa kuwa Fraser
alivalia kivazi hicho akijitofautisha na wenzake kutokana na kwamba alikuwa mkosefu licha ya kwamba alipokea madharau kutoka kwa wenzake huku wengine wakidhihaki vazi lake.
Fraser bado yuko kwa mkopo katika klabu hiyo akitokea katika klabu ya Bolton Wanderers, na alikumbana na adhabu ya kusimama michezo nane baada ya kushambuliana na mchezaji mwenzake wa Under-20 katika mchezo dhidi ya Dunfermline.
Fraser
anarejea kutoka kifungoni siku ya mwaka mpya ambapo watakuwa wakielekea kucheza dhidi ya Celtic, na inadhaniwa kuwa Thistle huenda akaongeza kipindi chake cha mkopo mpaka mwisho wa msimu.
Kitu kizuri kwa Fraser ni kwamab angalau katika kivazi chake hicho mguuni alivalia viatu vyeusi tofauti na hali ilivyo siku hizi hususani katika soka la England ambapo wachezaji wamekuwa na tabia ya kuvaa viatu vya marangi mengi.



Begani akilia: Fraser akifarijiwa na mchezaji mwenzake James Craigen (kushoto) wakati wa mazoezi

Fraser (kulia) alifungiwa kwa mchezo mbaya wa michuano ya Under-20 dhidi ya Dunfermline
No comments:
Post a Comment