Taarifa za hivi karibu zinaeleza kuwa kamati ya maandalizi inafanya mawasiliano na klabu ya Ashanti United ya Ilala jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuziba nafasi ya Yanga wakati huu ambapo michuano hiyo imepangwa kuanza kutimu vumbi hapo kesho.
Yanga ilikuwa imepangwa katika kundi C pamoja na Mabingwa
watetezi wa michuano hiyo Azam FC pamoja na
makamu bingwa Tusker ya Kenya na Unguja Combine.
Kwa
mujibu wa ratiba ya michuano hiyo, pazia la michuano hiyo litafunguliwa kwa mechi mbili za kundi B katika uwanja wa Amaan, ambapo wakati
wa saa 10:00 jioni ni mabaharia wa KMKM dhidi ya Kampala City Council (KCC) ya Uganda .
Aidha saa 2:00 usiku, wekundu wa Msimbazi Simba SC, watakuwa kibaruani dhidi ya AFC Leopards.
Januari 2, 2014, kutakuwa na mechi nne, katika kila uwanja, kati ya Amaan Unguja na Gombani Pemba, kutakuwa na michezo miwili.
Zile
za Amaan, ni kati ya Azam FC na Unguja Combine (saa 10:00 jioni) na
Yanga( Ashanti) dhidi ya Tusker itakayorindima kuanzia saa 2:00 usiku, na huko
Gombani shughuli itakuwa kati ya URA na Chuoni (kundi C) watakaovaana
saa 8:00 mchana, huku Mbeya City ikitoana jasho na Pemba Combine, saa
10:00 jioni katika mchezo wa kundi A.
Fainali
ya ngarambe hizo itapigwa uwanja Amaan Januari 12 wakati wa saa 2:00
usiku, ambayo ndiyo kilele cha maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
No comments:
Post a Comment