KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, December 28, 2013

PSG kuvunja rekodi ya dunia ua usajili kwa kumsajili Messi kwa pauni milioni 210.

Paris Saint-Germain ina mpango wa kuvunja rekodi ya dunia ya usajili wa pauni milioni £210 kwa ajili ya Lionel Messi.
Taarifa kutoka jijini Paris zinasema mabingwa hao wa ligi kuu ya nchini Ufaransa 'Liegue 1' wanataka kuvunja kibubu kwa ajili ya msambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kwa kuvunja mkataba wake na Barcelona.
Kwasasa mshambuliaji huyo anaonekana ni kama ni mwenye sintofahamu ndani ya Nou Camp kufuatia maoni ya mkurugenzi Javier Faus juu uboreshaji wa mkataba wake.

Wish you were here: Lionel Messi posted a picture of him and wife Antonella Roccuzzo in Rosario on Instagram
Lionel Messi akiwa katika picha ya pamoja na mkewe Antonella Roccuzzo mjini Rosario


Messi bado yuko katika mkataba wa pauni milioni £13.5 ambapo utamuweka katika klabu yake mpaka 2018 ambapo Faus alikaririwa akisema Messi huenda akapewa 'package bora' kufuatia ongezeko la pauni milioni £15 kwa mwaka kwa mshambuliaji wa timu pinzani Cristiano Ronaldo.

Messi aliyekuwa na hasira alikaririwa akisema 
'Faus ni mtu ambaye hajui lolote kuhusu soka na kwamba anataka kuiendesha Barelona kibiashara kitu ambacho sio sawa'

Endapo PSG watafanikiwa katika mpango huo itakuwa ni ada zaidi ya mara mbili ya rekodi ya uhamisho ya wachezaji duniani ambayo inashikiliwa na Gareth Bale ya pauni milioni £86.

Goals, goals, goals: Should Messi join PSG he would make up a stellar front three with Zlatan Ibrahimovic (below left) and Edinson Cavani (below right)

No comments:

Post a Comment