KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, December 28, 2013

Soma maoni ya mabadiliko ya sheria za sasa za soka kutoka kwa makocha wakubwa duniani huku maoni ya Cristiano Ronaldo ni noma....................

Mbadiliko ya sheria: Cristiano Ronaldo, akiongea mjini Dubai, amesema angependa kuona waamuzi kuweka ukuta umbali ya yard 10 kutoka eneo la pigo la huru la moja kwa moja. Alikuwa akijibu swali ya mwamuzi mkongwe Pierluigi Collina
Cristiano Ronaldo amewataka waamuzi duniani kote kuhakikisha wanawaweka wachezaji walinzi mbali na mpira wa adhabu ya moja kwa moja (free-kicks).
Nyota huyo wa Ureno na Real Madrid ni mmoja wa wapigaji wazuri wa pigo la aina hiyo duniani ambaye ametaka kufanyike mabadiliko ya sheria ambayo anadhani hiyo itamfanya aweze kuuzamisha mpira wavuni kupitia eneo la kona ya juu ya goli.

'Sheria ambayo itakuwa nzuri endapo itatumika popote ni kuwa wakati unapiga 'free-kick', mwamuzi aweke alama ya uzio kuhakikisha kuwa walizni wanakuwa mbali ' Amesema Ronaldo alipoulizwa katika mkutano wake na Dubai International Sports .

Ronaldo celebrates a goal against Sweden
Ronaldo lines up a free-kick

Pichani juu mshambuliaji wa Real Madrid na Ureno akijiweka tayari kupiga 'free-kick' na anaamini kuwa badiliko sheria hiyo itamuwezesha kufunga magoli zaidi kwa klabu na timu yake ya taifa.

Honour: Ronaldo was given the Global Soccer Award at the conference in Dubai
Tunzo: Ronaldo alikabidhiwa tunzo ya 'Global Soccer' katika mkutano wake mjini Dubai

NINI KINGINE WANGEPENDELEA KIBADILISHWE.

PEP GUARDIOLA, BAYERN MUNICH MANAGER
Kama kocha ningependelea kufanya mabadiliko mengi zaidi ya wachezaji, hii ingeniruhusu mimi kama meneja kuiongoza timun kwa uzuri zaidi. Itakuwa vizuri kuwa na wachezaji wengi  katika benchi kwa kweliIt. Kila mmoja angenufaika na hii kwasababu wachezaji wangekuwa wanachoka kidogo pia.

FABIO CAPELLO, RUSSIA MANAGER
Tungekuwa na muda kuongea na wachezaji kila baada ya muda fulani 'timeout'. Ukiwa katika benchi huwezi kuongea kubabilisha mbinu, huwezi kutuma ujumbe. Nchini Russia, endapo mchezaji anaanguka tunakuwa na dakika moja ya kusimamisha mchezo kuwapa wachezaji nafasi ya kupumua.Linazungumzika hili.

ANTONIO CONTE, JUVENTUS MANAGER
Fabio ameiba wazo langu. 'timeout' lingekuwa ni wazo zuri sana kwasababu ukiwa katika benchi huwezi kuwasiliana na wachezaji. Endapo utagundua makosa, dakika mbili za kupumzika kwa kutoa maelekezo zingefaa sana.
Ronaldo, mwenye magoli 40 katika jumla ya michezo 32 kwa klabu yake na timu ya taifa msimu huu alikuwa akiulizwa maswali na mwamuzi mstaafu na mkongwe Pierluigi Collina.

Pia alizwadiwa tunzo ya 'Global Soccer Award ' ya mwaka 2013 katika mkutano huo 'conference'.

Bahati nzuri katika maoni ya Ronaldo ni kwamba shirikisho la soka dunia FIFA hivi karibuni lilithibitisha kuwa waamuzi watakuwa wakipewa 'spray maalumu' katika kombe la dunia na hiyo bila shaka litakuwa ni jibu la maoni yake.

Wachezaji kadhaa na mameneja walikuwepo katika Conference hiyo iliyofanyika Dubai, akiwemo bosi ya Bayern Munich  Pep Guardiola, meneja wa Juventus Antonio Conte na yule wa and Russia Fabio Capello.
Magic marker: FIFA have decided to introduce biodegradable spray at the World Cup - it was successfully trialled in the Club World Cup in Morocco
Magic marker: FIFA imeamua kuanza kutumia 'biodegradable spray' katika kombe la dunia ilifanyiwa majaribio katika kombe la dunia la vilabu nchini Morocco
Brains trust: Juventus manager Antonio Conte (left), Russia manager Fabio Capello (centre) and Bayern boss Pep Guardiola all gave their opinion at the conference
Wanakuna vichwa: meneja wa Juventus Antonio Conte (kushoto), Meneja wa Russia Fabio Capello (katikati) na bosi wa Bayern Pep Guardiola wote walikuwa na maoni yao katika 'conference' hiyo
Audience: Former Real Madrid and Blackburn Rovers defender Michel Salgado was at the conference
Waalikwa: Mlinzi wa zamani wa Real Madrid na Blackburn Rovers Michel Salgado alikuwepo ndani ya conference


Hot stuff: Ronaldo has 40 goals in 32 matches for club and country this season

No comments:

Post a Comment