KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, January 25, 2014

Coastal Union yashindwa kuonyesha mambo ya Oman uwanja wa Mkwakwani dhidi ya JKT Oljoro

Yayo Kato akijishauri cha kufanya kabla ya kuanza kukimbizana na Ally Hamza wa JKT Oljoro.
Coastal Union ina mashabiki wa mataifa mengi.
Viongozi wa Coastal Union wakifuatilia mechi ya leo uwanja wa Mkwakwani.
Pamoja na kuweka kambi nchini Oman kwa wiki mbili, kikosi cha Coastal Union ya Tanga kimeshindwa kuwapa raha wapenzi wake katika uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga baada ya kulazimishwa sare na wanajeshi wa JKT Oljoro kutoka Arusha.
Suluhu ya 1-1 imeonekana kuwavunja nguvu viongozi na mashabiki wa Coastal Union, ambao waliingia uwanjani kwa idadi ndogo kutokana na tatizo la ukataji tiketi kuwakwaza baadhi ya mashabiki waliotaka kuiangalia timu yao iliyotoka Oman wiki hii.
Coastal Union walianza mchezo wa leo kwa kujiamini wakitoa pasi za uhakika huku wakifika katika lango la wapinzani wao mara kwa mara.
Kunako dakika ya 7, Yayo Kato aliandika bao la kwanza baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa Kenneth Masumbuko baada ya Hamad Juma kufanya kazi nzuri ya kumdhibiti beki wa Oljoro na kupiga krosi.
Bao hilo lilidumu kwa dakika 45 za awali ambapo mpaka timu zinakwenda mapumziko ubao uliendelea kusomeka 1-0. 
 
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku wachezaji wa Oljoro wakicheza kw akujihami na kupiga pasi fupi zilizoonyesha kuwachanganya wachezaji wa Coastal Union.
 
Kufikia dakika ya 75 Coastal Union, tayari walishafanya mabadiliko ya wachezaji watatu ambapo alitoka Kenneth Masumuko na kuingia Abdi Banda, baadae alitoka Othamn Tamim akaingia Crispian Odula mwisho alitoka Yayo Kato na kuingia Mohammed Miraji.
Wagosi wa Kaya waliendelea kumiliki mchezo na kumtumia zaidi Danny Lyanga alikuwa msumbufu katika winga ya kushoto na mara kadhaa kupiga hodi kwa mlinda mlango wa Oljoro, Mohammed Yusuf.
Ilipotimu dakika ya 87 dakika chache kabla ya mwamuzi wa leo Israel Nkongo kumaliza kipute, Hamis Saleh wa JKT Oljoro alitumia vema makosa ya mabeki wa Coastal Union na kupachika bao lililoamsha benchi la timu yake kwa furaha.
 
Dakika ya 89 Crispian Odula alipata pasi akiwa ndani ya 18 lakini akapiga shuti hafifu lililotua ndani ya mikono ya golikipa wa Oljoro.
 
Mpaka mchezo unakamilika, ubao ulisomeka 1-1 hali iliyowatoa kichwa chini wachezaji na mashabiki wa Wagosi wa Kaya waliokuwa na matumaini makubwa ya kushinda.

No comments:

Post a Comment