KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, January 25, 2014

Ligi kuu ya Ujerumani: Bayern Munich bado watamu Bundersliga

Bayern Munich imeanza duru ya pili ya Bundesliga kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Borussia Moenchengladbach jana Ijumaa baada ya mapumziko ya wiki tano ya majira ya baridi. 

Mario Goetze alifunga bao la kuongoza katika dakika ya saba ya mchezo, wakati walinzi wa Moenchengladbach walipomuacha bila ulinzi na kuupachika mpira wavuni , kabla ya Thomas Mueller kukamilisha ushindi wa bayern kutokana na mkwaju wa penalti katika dakika ya 54.

Granit Xhaka wa moenchengladbach alitumia mkono kuusimamisha mpira katika mtafaruku golini na ndipo refa akaamua mkwaju wa penalti kwa Bayern.
Bundesliga FC Bayern München Borussia Mönchengladbach Sport Deutschland Pambano kati ya Bayern dhidi ya Moenchengladbach

Moenchengladbach ambayo ilikuwa haijafungwa nyumbani msimu huu, ilifanikiwa  mara mbili kugonga mwamba wa goli la Bayern , wakati Max Kruse na patrick Herrmann waliopojaribu bahati yao dhidi ya kipa wa Bayern Manuel Neuer.

Matokeo hayo yameifanya Bayern kuendeleza ubabe wa kutofungwa katika Bundesliga kwa michezo 42 na sasa imepanua mwanya wa uongozi hadi point 10 ikifuatiwa na Bayer Leverkusen ambayo inacheza leo jioni dhidi ya Freiburg.

Mabingwa hao hata hivyo wana mchezo mmoja zaidi ambapo watacheza dhidi ya Stuttgart siku ya Jumatano ili kutimiza michezo 18 ya ligi ya Ujerumani Bundesliga hadi sasa.

"Iwapo tutacheza kama tulivyocheza leo tutakuwa mabingwa wa Ujerumani", amesema rais wa Bayern Uli Hoeness.
Zum Thema - Uli Hoeneß muss vor Gericht Rais wa Bayern Uli Hoeness

Mshambuliaji mashuhuri wa Bayern Mario Mandzukic hakuwamo katika kikosi hicho jana. Mkurugenzi wa sporti wa Bayern Munich Matthias Sammer amesema kabla ya mchezo huo kuwa mshambuliaji huyo kutoka Croatia hajafanya mazowezi vya kutosha.

Hakutaka kusema hata hivyo iwapo usajili wa Robert Lewandowski kutoka Borussia Dortmund kwa ajili ya msimu ujao una athari yoyote katika hilo.
Matokeo ya michezo ya leo 



Finished
Freiburg
Bayer Leverkusen
(1-2)





Finished
Wolfsburg
Hannover 96
(1-1)





Finished
Nurnberg
Hoffenheim
(2-0)





Finished
Borussia Dortmund
Augsburg
(1-0)





Finished
VfB Stuttgart
Mainz 05
(1-1)





25/01 20:30
Eintracht Frankfurt
Hertha Berlin 
 
Kesho(26.01.2014) ni zamu ya Werder Bremen itakayotiana kifuani na Eintracht Braunschweig na Schalke 04 iko ugenini dhidi ya Hamburg SV.
Bundesliga 1899 Hoffenheim Borussia Dortmund Wachezaji wa Borussia Dortmund wakipongezana baada ya kupata bao

Wakati huo huo Lukas Podolski aliweka mpira wavuni katika kipindi cha kwanza jana na kuisaidia Arsenal kuirarua Coventry ya daraja la tatu kwa mabao 4-0 katika mchezo wa duru ya nne ya kombe la FA.

Katika mchezo ambao Arsenal iliutawala toka mwanzo hadi mwisho, Podolski aliwainua mashabiki wa Arsenal katika dakika ya 15 kwa kufunga bao safi baada ya kumegewa pasi safi na Mesut Ozil. Aliongeza bao la pili kwa kichwa kunako dakika ya 27 ya mchezo.
Lukas Podolski Mshambuliaji wa Arsenal Lukas Podolski

Katika mchezo mwingine wa kombe la FA jana Ijumaa , Nottingham Forest ilitoka sare ya bila kufungana na Preston.

No comments:

Post a Comment