KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, January 15, 2014

Manchester United: Bye bye Luis Nani mlango uko wazi

 Manchester United sasa inajipanga kufungua mauzo ya mshambuliaji wa pembeni Luis Nani licha ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureni kuongeza mkataba na klabu hiyo majira ya kiangazi iliyopita.
David Moyes alikuwa chachu ya kumshawishi winga huyo mwenye umri wa miaka 27 kusaini mpango mpya uliokuwa na thamani ya euro €96,000 kwa wiki ndani ya Old Trafford, lakini sasa mambo yamemwendea kombo winga huyo kiasi klabu hiyo kuamua kufungua duka kwa ajili ya mauzo ya nyota huyo wa zamani wa Sporting Lisbon.
Mreno huyo msimu huu ameanza michezo minne tu, na hajaonekan uwanjani tena tangu mchezo wa mapema mwezi Disemba mwaka jana ambapo United ilipokea kichapo kutoka kwa Newcastle na tangu wakati huo amekuwa akiuguza majeraha ya msuli jambo ambalo limemfanya Moyes kutamka atamuweka pembeni kwa muda.

No comments:

Post a Comment