KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, January 15, 2014

Ramon Calderon: Cristiano Ronaldo hajazaliwa kuchezea Madrid,iko siku atarejea 'Premier League'

Rais wa zamani wa Real Madrid Ramon Calderon hadhani kuwa Cristiano Ronaldo anaweza kumalizia soka yake Santiago Bernabeu, huku akitarajia kuwa nyota huyo wa kimataifa wa Ureno anaweza kurejea 'Premier League' wakati wowote.

Ronaldo alitia saini mpango mpya na Los Blancos mapema mwanzoni mwa msimu, mpango ambao utamuweka hapo mpaka kiangazi 2018, ambapo pia Calderon bado anadhani kuwa mshambuliaji huyo atadhirisha kuwa ni bora zaidi kwa kadri siku zinavyozidi kwenda mbele.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alijiunga na Madrid akitokea Manchester United kiangazi 2009 na hivyo karibuni alitanabaisha wazi kuwa bado hajaisahau klabu yake ya zamani.

"Sidhani kama atamalizia soka yake ndani ya Real. nafikiria kuwa siku moja atarejea England," Calderon ameliambia gazeti la The Sun.

"Ndani ya Madrid, anafarijiwa na mashabiki, lakini mahusiano yake na Rais wa sasa Florentino Perez siyo mazuri kama alivyokuwa na Alex Ferguson wakati huo akiwa na Manchester United.

"Cristiano hakuzaliwa kuichezea Real Madrid. Kila mmoja duniani anataka kuwa na Cristiano katika timu yake"

Calderon alikuwa kiongozi wa Madrid kutoka mwaka 2006 mpaka 2009 kabla ya kumuachia Perez.

No comments:

Post a Comment