KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, January 14, 2014

Mcroatia Zdravko Logarusic auomba uongozi umpatie michezo miwili na timu za ndani na nje ya nchi.

Kocha mkuu wa wekundu wa Msimbazi Simba Mcroatia Zdravko Logarusic ameuomba uongozi wa wekundu hao kumpatia michezo miwili zaidi ya maandalizi kabla ya kuingia katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya soka Tanzania bara maarufu kama ligi kuu ya Vodacom.
Logarusic ameomba michezo hiyo ikiwa ni siku moja tu mara baada ya kurejea kutoka visiwani Zanzibar ambako Simba walikuwa wakishiriki michuano ya kuadhimisha miaka hamsini ya mapinduzi ya Zanzibar ambako Simba ilifanikiwa kufika fainali na kufungwa na KCC ya Uganda kwa bao 1-0.

Akiongea na Rockesports mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam, kocha msaidizi wa wekundu hao Selemani Matola amesema bosi wake ameuomba uongozi kumtafutia michezo miwili ya maandalizi zaidi, huku mchezo mmoja ukiwa na timu ya nchini Tanzania na mchezo mwingine dhidi ya timu kutoka nje ya nchi.
Matola amesema kimsingi wamekubali matokeo ya mchezo wa fainali na kwamba wanatengeneza kikosi kwa ajili ya ligi hivyo basi michezo hiyo itawasaidia kurekebisha makosa yaliyojitokeza kwenye michuano ya kombe la mapinduzi.  

No comments:

Post a Comment