Rais wa shirikisho la soka Tanzania Jamal Emil Malinzi |
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Symbion Power Tanzania Limited zimesaini
makubaliano ambapo kampuni hiyo itasaidia kwenye maeneo matatu ya mpira wa
miguu wa vijana.
Makubaliano
hayo yametiwa saini leo (Februari 26 mwaka huu) kwenye ofisi za TFF jijini Dar
es Salaam. Rais wa TFF, Jamal Malinzi amesaini kwa niaba ya shirikisho wakati
upande wa Symbion aliyesaini ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Peter Gathercoles.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ywa Symbion Peter Gathercoles. |
Maeneo
ambayo Symbion itasaidia ni ujenzi wa vituo viwili vya kuendeleza vipaji
vitakavyojengwa Kidongo Chekundu na Kinondoni mkoani Dar es Salaam, mashindano
ya Taifa ya wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 12 (U12) yatakayofanyika
mwaka huu na kuisaidia timu ya U17 ya Tanzania (Serengeti Boys).
Serengeti
Boys itacheza na Afrika Kusini, Julai mwaka huu katika mechi za mchujo kuwania
tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa wachezaji wa umri huo zitakazofanyika
mwakani nchini Niger.
Hivyo
Symbion imetoa dola 60,000 (zaidi ya sh. milioni 96) kwa ajili ya mashindano ya
U12, na dola 50,000 (zaidi ya sh. milioni 80) kwa ajili ya maandalizi ya
Serengeti Boys kwa mechi dhidi ya Afrika Kusini.
Rais
Malinzi ameishukuru Symbion kwa kukubali kushirikiana na TFF katika mpira wa
miguu wa vijana, lakini vilevile amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Jakaya Kikwete kwani ndiye chachu ya kampuni hiyo kuamua
kujishirikisha na mpira wa miguu wa vijana.
No comments:
Post a Comment