Kocha wa timu ya Taifa ya Uingereza, Roy Hodgson
amesema ana matumaini kuwa Brazil itahodhi kwa mafanikio michuano ya
kombe la dunia japo imekuwa ikikabiliwa na changamoto za viwanja na
maandamano.
Hodgson yuko kwenye ziara katika mji wa Manaus
nchini Brazil, ambapo timu ya Uingereza itachuana na Italia mjini humo,
lakini kuna hofu ya kutokamilika kwa uwanja wa Curitiba.
Kocha huyo ametoa wito kwa Fifa na Serikali ya Brazil kufanya jitihada kulikamilisha hilo.
Uwanja wa Arena Amazonia, haukua tayari ilipofikia tarehe iliyopangwa na Fifa ya tarehe 31 mwezi Desemba mwaka 2013.
Lakini katibu mkuu wa Fifa Jerome Valcke amesema
anafurahishwa na maendeleo ya uwanja huo, alipoutembelea mwishoni mwa
juma lililopita, maafisa hao wanasema uwanja umekamilika kwa kiasi cha
asilimia 97.
Michuano ya Kombe la dunia yanatarajiwa kuanza nchini humo tarehe12 mwezi Juni mwaka huu.
No comments:
Post a Comment