KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, June 18, 2014

Balotelli ananukia kwa washika mitutu msimu ujao posho ya wiki ni ya kupendeza

Mario Balotelli ni mlengwa mkubwa wa Arsenal (Picture: Getty)
Imeripotiwa kuwa Arsenal inajipanga kuweka mzigo mezani kwa ajili ya kupata huduma ya mshambuliaji Mario Balotelli ukiwa ni mpango unao husisha malipo ya wiki ya pauni £180,000 ili muradi tu ajiunge katika viunga vya Emirates msimu huu wa kiangazi.
Balotelli ni mmoja wa walengwa wa Gunners ambao meneja wake Arsene Wenger anaonekana kusaka kusaka mshambuliaji mkubwa mwenye kiwango cha dunia kwa ajili ya msimu ujao.
Mshambuliaji huyo wa AC Milan amefungua mlango wa mazungumzo ya uhamisho ambapo wakala wake amewaeleza wanahabari kuwa hilo linaweza kutokea kwani kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 27 katika wiki chache zijazo.

Hata hivyo Arsenal bado haijafanya mazungumzo rasmi lakini taarifa nchini Italia zinasema kuwa maafisa wakubwa akiwemo kiongozi wa mapatano Richard Law amesema kuna mpango wa awali wa malipo ya £180,000 kwa wiki kwa Balotelli endapo mpango huo utafanikiwa.
Kwasasa ndani ya AC Milan Balotelli anakunja kiasi cha pauni  £150,000 kwa wiki.