Ghana iliyocharazwa na Marekani mabao mawili kwa moja dhidi ya Marekani katika mechi yao ya kwanza |
Shirikisho la soka nchini Ghana,
limekanusha ripoti za kituo kimoja cha redio nchini humo kwamba timu ya
taifa ambayo inashiriki michuano ya kombe la dunia imekumbwa na
mgawanyiko hasa baada ya kushindwa na Marekani mabao mawili kwa moja
Jumatatu.
Kulingana na kituo hicho cha Joy FM, huenda
wachezaji wamegawanyika na kumkataa kocha mkuu, hali ambayo ililazimisha
maafisa wa timu hiyo kufutilia mbali mkutano waliokuwa wameandaa na
waandishi wa habari Jumanne.
Shirikisho hilo limesema: ''Tunataka kuthibitisha kuwa ripoti hizo sio za kweli na hazina ushahidi wowote.''
"hakuna mchezaji hata mmoja ametofautiana na kocha Kwesi Appiah."
Wachezaji wanajiandaa kwa mechi nyingine Alhamisi ijayo
Taarifa hiyo iliongeza kusema, "hakuna mchezaji
au wachezaji wamehusika na njama ya kukataa kucheza pamoja na kumpinga
kocha mkuu. ''
"mkutano ambao tulikuwa tumeandaa na wandishi wa
habari ambao ulipangwa kufanyika saa tano saa za Brazil, ulikuwa wa
wasimamizi wa timu wala sio wachezaji. Ulibadilishiwa muda na kupangwa
kufanyika saa kumi na nusu jioni kwa sababu kikosi kilikuwa kimeswali
kuchelewa.''
Wachezaji wote 23 wa timu ya taifa ya Black Stars, walikuwepo tayari kwa mkutano kwa mwongozo wa Appiah.
Tunataka kuwahakikishia wananchi wa Ghana kuwa
kocha Kwesi Appiah na wachezaji wake, wanaangazia zaidi mechi yao dhidi
ya Ujerumani wiki ijayo, na wako makini kushinda mechi hiyo.
Baada ya mechi ya Ujerumani, mechi ya mwisho ya Ghana itakuwa dhidi ya Portugal Alhamisi wiki ijayo.
No comments:
Post a Comment