KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, June 18, 2014

Wesley Sneijder: Hakuna mtu ndani ya uholanzi anaye mkataa Louis van Gaal, nitafikiria ofa yake ya kujiunga na United

Nyota wa timu ya taifa ya Uholanzi kiungo Wesley Sneijder amesema atafikiria juu ya suala la kuhamia Manchester United endapo meneja wa mpya wa klabu hiyo ambaye pia ni kocha wa kikosi cha Uholanzi Louis van Gaal atataka ajiunge naye.
Kiungo huyo wa Galatasaray alikuwa akihusishwa na Old Trafford misimu kadhaa iliyopita jambo ambalo halikufanyiwa kazi.
Hata kiungo huyo wa zamani wa Inter Milan amesema anaweza kujiunga na mashetani wekundu ambapo inafundishwa na mduchi mwenzake baada ya kumalizika kwa fainali ya kombe la dunia akisubiri kama kutakuwa na mpango huo.

‘Ndani ya Netherlands, Van Gaal ni kitu kama mwalimu mkuu wa shule’ amesema Sneijder.
‘Si kila mtu anapata bahati ya kujiunga naye katika kitabu chake.

‘Anawafundisha wachezaji kwa kila hali na siku zote anategemea kiwango cha juu.
‘Ninafuraha ndani ya Galatasaray, nimejiimarisha ndani ya klabu na nimetulia.
‘Pamoja na hilo kama  Van Gaal ataonyesha kunitaka, nitajiweka katika nafasi ya kufikiria juu ya hilo. Hakuna mtu ndani ya Netherlands anaye mkataa Van Gaal.’