KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, June 14, 2014

David Luiz ajiunga na PSG kwa uhamisho mnono

David Luiz amekamilisha uhamisho kutoka Chelsea na kujiunga na Paris St Germain ambapo nyota huyo wa kimataifa wa Brazil amesaini mkataba wa miaka mitano na bingwa huyo wa Ufaransa.

Luiz ambaye aling'ara akiwa na kikosi cha Brazil maarufu kama Selecao katika mchezo wa ufunguzi wa fainali ya kombe la dunia kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Croatia alhamisi usiku ameondoka Stamford Bridge kwa ada kubwa ya uhamisho ya pauni milioni £50.
PSG imetangaza mpango huo kupitia mtandao rasmi wa klabu ikisema 
'Paris Saint-Germain is delighted to announce the transfer of Brazilian international David Luiz from Chelsea FC, for the next five years.'

Luiz alijunga na  Chelsea akitokea Benfica January 2011.