KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, June 14, 2014

Mourinho achague kumsajili Thibauti Courtois lakini Petr Cech asugue benchi

GOLIKIPA Thibaut Courtois ameipa masharti klabu yake ya Chelsea ikiwa ni hatma yake kuwa ifanye maamuzi magumu ya kumfanya yeye kuwa mlinda mlango nambari moja ka si hivyo badi wamruhusu aende zake Atletico Madrid.

Mlinda mlango huyo raia wa Belgium ambaye alikuwa msaada mkubwa kwa Los Colchoneros katika ligi ya Hispania La Liga katika kipindi chake kirefu cha kuwepo kwa mkopo msimu uliopita, amesema hatma yake ya baadaye haitakuwa sawa mpaka fainali za kombe la dunia litakapo malizika.

Meneja wa Chelsea Jose Mourinho yupo katika mipango ya kumsajili mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 22 kujiunga Stamford Bridge msimu ujao lakini Courtois amesema atarejea tu endapo atakuwa chaguo la kwanza mbele ya Petr Cech.

‘Do I want to be number one wherever I play next season? Yes, I think with my age and the performances I had I want to play,’ Amesema Courtois, ambaye amechezea michezo 56 Atletico msimu uliopita.