KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, June 14, 2014

Kuelekea mchezo dhidi ya England kikosi cha Italia kinakabiliwa na majeruhi wa kutosha

Gianluigi Buffon atakuwa nje  ya kikosi cha timu ya taifa ya Italia katika mchezo wa ufunguzi wa kombe la dunia dhidi ya England.
Mlinda mlango huyo wa Juventus amejikuta akipata majeraha akiwa mazoezini hapo jana alipotonesha enka na hivyo kushindwa kumalizia mazoezi katika uwanja wa Manaus.

Mlinda mlango huyo aliyekuwepo katika kikosi cha ushindi wa kombe la dunia 2006 hayuko vizuri kuanza hii leo na hivyo kutoa nafasi kwa mlinda mlango wa Paris Saint-Germain Salvatore Sirigu kuchukua nafasi yake.
Buffon ametupia ujumbe wa kutia moyo kupitia ukurasa wake wa Tweeter akisema: 'kuna njia nyingi za kuwa muhimu hata kama hauko katika nafasi ya kuanza ... so... come on Salvatore, come on magical boys.'
Prandelli anatatizo lingine la kikosi cha kwanza ambapo mchezaji mlinzi wa kushoto chaguo la kwanza wa AC Milan Mattia di Sciglio, ana majeraha aliyoyapata akiwa mazoezini alhamisi.

Haijawa wazi kama Italia itakuwa vizuri kwa kumtumia mlinzi wa Torino Matteo Darmian kushoto na kumtumia Ignazio Abate wa AC Milan ulinzi wa kulia au kama atatumika Giorgio Chiellini pembeni badala ya ulinzi wa kati huku mlinzi wa kati wa Parma akisogezwa sehemu ya kiungo.