Mgomo wa wafanyakazi wa treni ya chini ya ardhi mjini Sao Paulo |
Fainali za kombe la dunia zinakaribia kuanza hapo Alhamis wiki hii, huku
kukiwa na mchanganyiko usiokuwa wa kawaida wa hali yenye utata kwa
wenyeji Brazil na shirikisho linaloendesha mchezo huo FIFA
Majira ya baridi mjini Rio de Janeiro huambatana na hali isiyotabirika,
kuna baadhi ya siku jua ni kali na unyevunyevu wenye joto kali, katika
wakati wa kuelekea ufunguzi wa michezo ya fainali za kombe la dunia ,
ambalo linaweza kuwa , kimbunga kikali, cha kisiasa, kijamii na wasi
wasi katika soka, ingawa huenda ni Brazil pekee inayoweza kuizusha hali
hiyo.
Uwanja wa Maracana , utakaotumika kwa fainali ya Julai 13, ni mahali
sahihi kwa ajili ya maadili na mabadiliko ya fainali hizi nchini Brazil.
Wakati jioni ikiingia , uwanja huo hung'ara kwa taa za rangi ya
kijani na njano katika paa lake, wakati jua likichomoza , eneo hilo
linalozunguka uwanja huo huonekana limepooza na lisilokuwa na maana,
likiwa na wafanyakazi 20 tu wakishughulika kufunga nyaya za umeme katika
mtaa.
Brazil sio nchi ya "mambumbumbu"
Brazil sio nchi kwa ajili ya watu wasiojua kitu, amesema mtunzi na
mwimbaji maheremu Tom Jobim, mmoja kati ya vitu vya kufikirika katika
nchi hiyo kubwa katika America ya kusini.
Jobim huenda angesema pia kuwa Brazil sio nchi kwa ajili ya Waswisi ,
kwasababu moja kati ya matatizo ya kombe la dunia ni tofauti za
kitamaduni kati ya wataalamu na FIFA yenye makao yake makuu nchini
Uswisi na nchi ambayo , kwa kusema kweli, inafanya shughuli zake tofauti
kabisa.
Iwapo FIFA iliweza kuchukua kombe la dunia lililofanyika nchini Afrika
kusini mwaka 2010 na kuwa watayarishaji wa fainali hizo, ambazo zilikuwa
bora zaidi kuliko walivyotarajia watu wengi kutoka bara la Ulaya , hii
ni kutokana na kwamba Watu wa Afrika kusini waliridhika tu na kuwa
wenyeji wa kombe la dunia katika bara la Afrika.
Walijisikia kwamba hawahitaji mambo zaidi, waliishukuru FIFA.
Hata hivyo , Brazil ni tofauti, kwa sababu ya historia yake na kujisia
fahari , pamoja na nguvu kubwa za kiuchumi licha ya hali ya mparaganyiko
iliyopo. Brazil haihisi kuishukuru FIFA kabisa. Kuanzia rais Dilma
Rousseff hadi chini, Wabrazil wanahisi kwamba FIFA inapaswa kutoa
shukrani kwa Brazil, kwa kuzileta fainali hizo kwa kile kinachojulikana
kama " taifa la soka".
Kwa hiyo hamasa ni kubwa , isiyotabirika na bila kuwa na hakika ya mwisho wake.
Mgomo watishia kuleta mparaganyiko katika usafiri
Wafanyakazi wa treni ya chini ya ardhi mjini Sao Paulo wamekaidi uamuzi
wa mahakama jana Jumapili na wanaendelea na mgomo wao unaotishia
kusababisha mtafaruku katika usafiri wakati wa mchezo wa ufunguzi mjini
humo ambapo Brazil itapambana na Croatia.
Wafanyakazi hao wamepiga kura kuendelea na mgomo wao saa kadhaa baada ya
mahakama ya kazi kuamua kuwa ni kinyume na sheria na kuwatoza faini ya
dola 222,000 kwa kila siku watakayoshindwa kuripoti kazini.
Mgomo huo umekwisha sababisha misururu mirefu ya magari katika mji huo
wenye wakaazi milioni 20 wakati uwanja mpya wa mji huo unajitayarisha
kuwapokea mashabiki 60,000 katika mchezo huo wa ufunguzi siku ya
Alhamis.
No comments:
Post a Comment