KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, June 10, 2014

Mtibwa sugar kusaka wachezaji mchangani kukimbia gharama

Kocha mkuu wa Mtibwa Sukari Meck Mexime amesema katika kipindi hiki hawatofanya utaratibu wa kufanya usajili wa wachezaji kwa kutumia ghama kubwa ya fedha kama ilivyo kwenye klabu nyingine za ligi kuu ya soka Tanzania bara.

Mexime ambae amesema anaamini wachezaji chipukizi wataweza kukisaidia kikosi chake katika mshike mshike wa ligi kuu ya soka Tanzania bara, baada ya kubaini wanahitaji kuaminiwa kama ilivyo kwa wachezaji waliozeleka.

Mecky ambaye kwasasa yuko darasani amesisitiza kuwa wao kama Mtibwa Sugar hawako tayari tena kutumia kikubwa cha fedha wakiamini ya kuwa msimu ujao watakuwa na timu ya upinzani kuwania ubingwa wa ligi kuu unaoshikiliwa na klabu ya Azam fc.