Makamu wa Rais wa TFF Wallace Karia |
Makamu wa Rais wa Shirikisho la soka nchini TFF,
Wallace Karia hii leo amezindua kozi ya Leseni B inayotambuliwa na Shirikisho
la barani Afrika CAF.
Wallace
Karia amezindua kozi hiyo inayoshirikisha makocha zaidi ya 20 wenye Leseni C
kutoka Tanzania Bara pamoja na Zanzibar chini ya wakufunzi wanaotambuliwa na
shirikisho la soka barani Afrika CAF
Sunday Kayuni pamoja na Salum Madadi ambae ni mkurugenzi
wa Ufundi wa TFF.
Karia amewataka makocha wanaoshiriki katika kosi hiyo
kuwa wasikivu kwa ajili ya kupata elimu ya soka ambayo itakuwa kichocheo
kikubwa katika maendeleo ya mchezo huo hapa nchini.
Nae mkufunzi mkuu katika kozi hiyo Sunday Kayuni Amesema
anaamini mafunzo yatakayotolewa katika kizo hiyo inayofanyika jijini Dar es
salaam itakuwa ni motisha kwa makocha washiriki kwenda kuendeleza elimu katika
vilabu vyao ili kutimila malengo yanayokusudiwa na shirikisho la soka nchini
TFF.
Kwa upande wa washiriki ambao waliwakilishwa na kocha kituo
cha kulea na kuendeleza vipaji kwa vijana cha wakati ujao Wane Nelson Mkisi
amesema hawana budi kuyafanyia kazi wanayojifunza katika kozi hiyo, hivyo
amemuahidi makamu wa raisi wa TFF Wales Karina kutarajia mabadiliko siku za
usoni.
No comments:
Post a Comment