KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, June 18, 2014

Viongozi wa matawi Yanga waitaka kamati ya utendaji kuwasimamisha wanachama wanao hoji uvunjifu wa katiba

Viongozi wa Matawi ya Yanga wakiongozwa na Mohamed Msumi (wa kwanza kulia) . Picha na Gervas Mwatebela - See more at: http://shaffihdauda.com/?p=2282#sthash.ayFJyIIM.dpuf
Viongzi wa matawi ya Yanga wameitaka kamati ya utengaji ya klabu hiyo kuwasimamisha uanachama wanachama wake ambao wanagomea maamuzi ya mkutano mkuu wa klabu hiyo ambayo yalikiuka katiba ya klabu hiyo kwa kuwaongezea muda wa uongozi viongozi walioko madarakani.
Akiongea kwa niaba ya viongozi wa matawi ya klabu hiyo katika makao makuu ya klabu hiyo, mwenyekiti wa matawi Mohamed Msumi ambaye alikuwa pamoja na wazee wa klabu hiyo Jabir Katundu na Mzee Akilimali, Msumi amesema kitendo cha wanachama hao kupiga hodi shirikisho la soka nchini TFF kuhoji uhalali wa maamuzi ya mkutano mkuu wa Juni mosi ni kujaribu kutaka kuleta vurugu ndani ya klabu hiyo ambayo kwasasa wanajaribu kujenga timu kwa kufanya usajili ikiwa ni maandalizi ya msimu uajao wa ligi.
Msumi ameitaka kamati ya utendaji ya klabu hiyo inayoongozwa na mwenyekiti wake Yusufu Manji kuwasimamisha uanachama wanachama hao bila kwani wanatishi kuvunja amani ndani ya klabu hiyo.