Wachezaji wa Tanzania walioko Uholanzi, Dickson
Ambundo na Shiza Yahya wameanza kuonekana muda na waandaaji
ya mashindano ya AEGON Copa Amsterdam.
Kwa mujibu wa wakala wa wachezaji wa Uholanzi, Denis Kadito,
AEGON Copa Amsterdam ni mashindano ya kimataifa yanayoshirikisha timu kubwa
kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni kwa wachezaji wa miaka chini ya 19.
Kwa Uholanzi, Ajax Amsterdam huwa lazima washiriki, na pia
huwa kuna timu ya ridhaa inayotengenezwa kwa kuchagua “best talent” kutoka
Uholanzi. Mchujo wa wachezaji hao kutengeneza timu ya kombaini, ulianza na
wachezaji wasiopungua 1,000.
Kombaini hiyo inaitwa Men United na inafundishwa na mchezaji
wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi, Ronald de Boer. Ronald e Boer ni pacha wa
kocha wa Ajax (First team).
Ronald de Boer pia ni kocha wa wachezaji washambuliaji wa
Ajax. Shiza na Ambundo waliingizwa kwenye mchujo na wakafanya vizuri, mwishoni
wakaitwa kwenye timu ya wachezaji 18 waliotengeneza timu ya Men United. Hii ni mara
ya kwanza wachezaji wasio Waholanzi kuingizwa katika timu hiyo.
Mashindano ya Copa Amsterdam yameanza juzi (Juni 8 mwaka
huu) na yanaisha kesho (Juni 11 mwaka huu. Katika mashindano hayo kuna makundi
mawili. Kundi A ni AFC Ajax (Amsterdam), Ajax Cape Town ( Afrika Kusini),
Fluminense (Brazil), Hamburg SV (Ujerumani) wakati B ni Men United, Panathinaikos
(Ugiriki), FC Aerbin (China) na Cruizero (Brazil).
Shiza na Ambundo wamecheza mechi zote tatu. Shiza amekuwa
akicheza namba tatu wakati Ambundo anapiga namba tisa, saba na kumi na moja.
No comments:
Post a Comment