Chama cha soka nchini Uingereza FA, kimeidhinisha matumizi
ya Vanishing Spray, kuanzia msimu ujao wa ligi kuu ya soka nchini humo pamoja
na michuano mingine iliyo chini ya chama hicho.
FA wamekubali matumizi ya Vanishing Spray, baada ya
majadilino na chama cha waamuzi nchini Uingereza ambacho kimeafiki matumizi ya
Spray hiyo ambayo mashabiki wengi walianza kuiona wakati wa fainali za kombe la
dunia zilizofanyika nchini Brazil.
Tayari nchi kama Hispania pamoja na Italia zimeshathibitisha
matumizi ya Vanishing Spray, hivyo Uingereza inakuwa nchi ya tatu barani Ulaya
kukubali waamuzi kutumumia mfumo huo.
Mtendaji mkuu wa chama cha soka nchini Uingereza FA Richard
Scudamore, amesema imewalazimu kupitisha Vanishing Spray, kwa lengo la kupiga
hatua ambapo wanaamini malalamiko huenda yakapungua kutoka kwa wachezaji pamoja
na mameneja ambao wamekua wakipingana na waamuzi inapotokea adhabu ndogo.
Kutokana na maazimio hayo, Uingereza wanakubali kusudio la
pili kutoka shirikisho la soka duniani FIFA la kumaliza utata uwanjani baada ya
kufanya hivyo wakati wakipitisha matumizi ya mfumo wa utambuzi wa mpira kuvuka
mstari wa goli *Goal Line Tecknology* ambao ulianza kutumika kwenye ligi ya
nchini humo msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment