KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, July 31, 2014

Michuano ya Kagame: 99% Niyonzima, Kiiza na Okwi nje

Haruna Niyonzima na Hamisi Kiiza mashakani michuano ya Kagame
Wakati michuano ya vilabu bingwa Afrika mashariki na kati maarufu kama kombe la Kagame ikitarajiwa kuanza Agosti 8 2014 jijini Kigali, kuna kila uwezekano wa kocha mkuu wa klabu ya Yanga M-brazil Marcio Maximo kuwapiga chini wachezaji Haruna Niyonzima, Hamisi Kiiza na Emmanuel Okwi kutokushiriki michezo ya michuano hiyo kutokana na na kile kinacho elezwa kuwa tangu alipowasili klabu hapo kwa kandarasi ya kukinoa kikosi hicho kwa mkataba wa miaka miwili bado kocha hajafanikiwa kuwaona nyota hao.
Akiongea na mtandao wa Rockersports.com katibu mkuu wa klabu hiyo Beno Njovu amesema kocha Maximo bado ameendelea kusisitiza kuwatumia wachezaji alionao kambini kwasasa wakati huu ambapo wanajiandaa na michuano hiyo na ligi kuu ya soka Tanzania bara kwani amekwisha kuwafahamu vema akiwa nao mazoezini.
Njovu amesema nafasi ya Maximo kwasasa kuwaona wachezaji hao wa kigeni kutoka Uganda na Rwanda kabla ya michuano ya Kagame Cup kule Rwanda imezidi kuwa finyu kwasasa kwakuwa wachezaji hao bado wako katika vikosi vya timu zao za taifa ambazo zitakuwa na majukumu ya kimataifa Agosti 2 na 3 na kwamba muda huo ni mfupi kwao kuweza kurejea Dar es Salaam kwa maandalizi ya kulekea Kigali.
Rwanda wanatarajiwa kukutana dhidi ya Congo Agosti 2,  wakati Tanzania na Uganda wakitarajiwa kucheza dhidi ya Msumbiji na Mauritania Ugenini.
Emmanuel Okwi
Kufuatia Yanga kuwasajili wachezaji  wawili kutoka nchini Brazil msimu huu Andrey Coutinho na Santos Santana ‘Jaja’ hali imekuwa tete juu ya hatma ya wachezaji Haruna Niyonzima, Hamisi kiiza Diego na Emmanuel Okwi ambao mmoja kati yao lazima afutwe ajira yake klabuni hapo, kutokana na kanuni ya usajili kuibana klabu hiyo ambayo kwasasa inawachezaji sita huku kanuni hiyo ikitamka klabu kusajili wachezaji watano wa kigeni.
Beno Njovu amethibitisha kuwa Yanga itaondoka nchini kabla ya Agosti 5 2014 tarehe ambayo si rahisi kwa akina Kiiza, Niyonzima na Okwi hawajatua nchi kuungana na wenzao kwa safari ya Kigali.
Ingawa Haruna Niyonzima atapata nafasi ya kuungana na wenzake akiwa Kigali bado nafasi yake inaonekana kuwa ngumu wakati wa michuano hiyo kwani Maximo hatakuwa tayari kumtumia kiungo huyo ambaye hakuwahi kuwa naye hapo kabla.
Yanga imepangwa katika kundi A pamoja na vilabu vya Rayol ya Rwanda, KMKM ya Zanzibar, Atlabara ya Sudani kusini na Coffee ya Ethiopia ambapo wataanza kampeni ya kuwania taji hilo dhidi ya wenyeji Rayol Sports Agosti 8 uwanja wa Amahoro.

No comments:

Post a Comment